• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nafasi ya Bunge kwenye mgogoro wa kibishara China na Marekani

    (GMT+08:00) 2019-03-01 09:29:29

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    MSUGUANO wa kibiashara kati ya China na Marekani umeingia mwaka wa pili sasa. Hali ya kutoelewana ulianza mwaka 2017.

    Bunge la Umma la China linaketi ikiwa msuguano huu haujapata ufumbuzi wa kudumu pamoja na kuwepo kwa hatua na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na pande zote mbili.

    Wachambuzi wa mambo ya kiuchumi na kidiplomasia wanaamini kwamba njia pekee ya kupata suluhu la kudumu ni pande zote –China na Marekani kuwa na uwanja sawa wa kibiashara.

    Bunge la umma la China ni chombo chenye madaraka ya juu kabisa la taifa, ambalo linaundwa na wajumbe waliochaguliwa kutoka mikoa, mikoa inayojiendesha, miji inayotawaliwa moja kwa moja na serikali kuu, mikoa ya utawala maalum na jeshi.

    Chombo hicho kinaendesha madaraka ya taifa ya utungaji wa sheria na kuamua masuala makubwa ya maisha ya siasa ya taifa.

    Kwa kutambua hili na majukumu yake ya msingi ya kuangalia mustakabali mzima wa taifa katika nyanja zote za kijamii, kiuchumi na kisiasa, suala la msuguano huu wa kibiashara ni muda muafaka pia ukalitupia jicho na kushauri serikali namna bora ya kulitatua kwani bila ufumbuzi wa haraka litakuwa na athari kubwa zaidi, si kwa China na Marekani pekee, bali kwa dunia nzima kwa ujumla.

    Pamoja na madaraka mengine iliyonayo Bunge la Umma la China, chombo hiki kina majukumu ya kuidhinisha mipango ya maendeleo ya uchumi na kuishauri serikali katika masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

    Kiuchumi, Marekani inaongoza duniani ikifuatiwa na China ambayo ilipanda kutoka namba sita hadi kuwa namba mbili duniani bila kwenda hatua kwa hatua kama zilivyofanya nchi nyingine wakati wa kupanda.

    Ni dhahiri kuwa matatizo yoyote yanayohusisha haya mataifa mawili yanakua na athari kubwa kwa uchumi wa dunia, hivyo ni muhimu vyombo vinavyohusika kuchukua hatua ya dharura na ya mapema.

    Ustawi wa haraka wa uchumi wa China na kadhalika nafasi ya nchi hiyo katika biashara ya dunia ni mambo ambayo yanapaswa kutiliwa maanani wakati wa kuchunguza chanzo cha tofauti zilizopo kati ya yake na Marekani.

    Kwa sasa China imekuwa mshindani mkubwa wa Marekani, hivyo basi, ustawi wa uchumi wa nchi hiyo duniani unawatia wasiwasi mkubwa viongozi wa Marekani.

    Wataalamu, wanaona kwamba kwa sasa Wamarekani wanatambua kwamba nafasi ya juu ya uchumi na biashara ya China na kadhalika ushirikiano wake na nchi mbalimbali za dunia, vina madhara kwa Marekani na kwa sababu hiyo wameamua kukabiliana na nao.

    Makabiliano ya kibiashara kati ya Marekani na China, yaliibuka kufuatia uamuzi wa Rais Donald Trump wa Marekani kuzipandishia kodi ya ushuru wa forodha bidhaa za China zinazoingizwa nchini humo ikiwemo, aluminiamu na chuma.

    Kufuatia hatua hiyo ya Marekani, China nayo ililipiza kisasi kwa kuzipandishia ushuru wa forodha za nchi hiyo, suala ambalo liliwalazimisha viongozi wa Marekani kuwasilisha mashitaka katika Shirika la Biashara Duniani (WTO).

    Tayari, Taasisi ya Fitch Ratings inayojishughulisha na ukusanyaji maoni ya mambo ya kiuchumi, pamoja na wachambuzi mbalimbali wamemetabiri kwamba, mgogoro wa kibiashara kati ya Marekani na China utakuwa mkubwa zaidi kama hatua ya haraka isipochukuliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako