• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaihakikishia dunia kuwa uchumi wake upo imara

    (GMT+08:00) 2019-03-06 08:39:51

    NA VICTOR ONYANGO

    BEIJING, CHINA

    Hivi karibuni kumekuwa na wasiwasi miongoni mwa nchi mbali mbali ulimwenguni kuhusiana na kuzorota kwa uchumi nchi wa China ambayo ni ya pili duniani kuwa na uchumi bora baada ya Marekani.

    Lakini wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wabunge siku ya jumanne, waziri mkuu Li Keqiang kupitia kwenye ripoti ya kazi ya serikali alihakikishhia wenyeji na ulimwengu mzima kuwa uchumi wa China hujazorota na kuna mipango kabambe za kudhibiti uchumi wa nchi.

    Kulingana na bwana Li, serikali inania ya kujiingiza kwenye maendeleo wa ubora wa juu nchini na nje ya China mwakani kwa manufaa wa uchumi wa dunia.

    Ripoti ya kazi ya serikali inadhihirisha kwamba nchi ya China inatarajia upato wake uhimarika na asilimia sita nukta tanu mwaka huu ili kuthibiti hali yake ya uchumi ilhali hatua hiyo itakumbwa na changamoto si haba.

    "Kama serikali, tuna matumaini kuwa pato la nchi (GDP) itanawiri mwaka huu kwa asilimia sita nukta tano ata kama kuna changamoto nyingi ambazo zinakandamiza uchumi ulimwenguni.China pia itaendelea kushirikiana na nchi mbali mbali na kufuata kanuni kadhaa kuhusu njia ya kukuza upato wa nchi," bw waziri mkuu kasema.

    Bwana Li alieleza kongamano uliyo hudhuriwa na rais wa nchi bwana Xi Jinping kuwa serikali kuwa pato la nchi ilifika kiwango cha asilimia sita nukta sita baada ya serikali kupitia mwongozo wa rais kutarajia asilimia sita nukta moja.

    China pia unapanga kuondoa karibu dola za Marekani 298.3 billioni kwenye ushuru kwa mnajili wa kuimarisha sekta ya watu wenyewe na viwanda vya chini kwa njia moja wapo wa kuimarisha uchumi wa nchi.

    "Ili serikali ikuze pato lake, kanuni zetu kuhusu pesa lazima ziwe zile ambazo zinaunga usambazaji wa pesa nchini kwa mundo mzingi wa kukuza uchumi wetu," ripoti yaeleza.

    Kwa mnajili wa kulinda na kukuza mazingira ya kibiashara nchini China, serikali inapanaga kufanya kampeni dhidi ya bidhaa gushi na kufanya mabadiliko kwenye sheria ya uwekezaji wa kigeni.

    Nchi ya Uchina kuendelea na mpango wake wa kidiplomasia kwa kupitia mpango wake wa kufadhili ujenzi mbali mbali wa barabara katika nchi tofauti tofauti kama njia ya kuendelea kufanya biashara pamoja na nchi za nje ili kuboresha uchumi wake.

    "Baada ya kuandaa kongamano uliyoleta rais mbali mbali ili kujadili mpango wa Uchina kudhamini ujenzi wa barabara mbali mbali, mwaka huu tutaandaa kikao cha pila ya Belt and Road Forum for International (BRI) ili tuboreshe ushirikiano wetu na nchi zingine kwa mnajili wa faida ya pande zote," bwa waziri mkuu aeleza.

    Serikali pia imesisitiza kuwa imepiga hatua kadhaa kushughulikia swala cheti ya ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana na kuahidi kuwa mwaka huu, wataweka kando nafasi millioni kumi na moja za kazi ili kuhakikisha ukosefu wa kazi mjini unabaki kwenye kiwango cha asilimia tano nukta moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako