Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM
MWAKA huu China na Tanzania zinaadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa kibalozi huku uhusiano huo ukiwa umedumu kwa amani na kusaidia katika Uhusiano katika sekta mbalimbali ikiwemo kifedha, Kibiashara, Utamaduni, miundombinu, utalii na mengineyo.
Kutokana kuimsrika kwa Ushirikiano kwa miaka mengi China imekuwa ikiongoza kwa kuweka mitaji mikubwa nchini Tanzania kwa zaidi ya dola Bilioni 5.8 Duniani katika uwekezaji kuanzia mwaka 1990 mpaka 2017.
Inaelezwa kuwa China ina miradi 723 ikitoa ajira 87,126 kwa thamani ya dola Milioni 5 962.74, ikifuatiwa na Uingereza yenye miradi 936 iliyozaa ajira 274,401 kwa thamani ya dola Milioni 5,540.07 na Marekani ikiwa na miradi 244 iliyozalisha ajira 51,880 kwa thamani ya dola Milioni 4,721.15.
Takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) zimebainisha kuwa China inaendelea kuwa nchi yenye lengo la kuwekeza zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, viwanda, utalii, Ujenzi, Teknolojia ya Mawasiliano na nyinginezo.
Katika kuimarisha uhusiano katika Nyanja za Utalii Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) na Kampuni ya Touchroad International Holdings Group (TIHG) ya nchini China wamesaini mkataba wa kufanya majadiliano ya kibiashara ya namna ya kuwasafirisha watalii zaidi ya 10,000 wanaotarajia kuingia nchini Tanzania mwaka 2019.
Awali, TIHG ilisaini mkataba na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) ya kuleta watalii hao 10,000 mwaka jana kwa kutumia ndege zake, hivyo utiaji saini wa mkataba huo na ATCL ni mwendelezo utekelezaji wake kwa kampuni hiyo kuwaleta nchini watalii kutoka China kisha watalii hao watatumia ndege za ATCL kuelekea maeneo mbalimbali ya utalii nchini.
Mwenyekiti wa TTB, Jaji Thomas Mihayo anasema katika kuhakikisha sekta ya utalii inakuwa na mchango mkubwa katika uchumi, imeanza kutekeleza makubaliano ya kuleta watalii 10,000 nchini.
Anasema wanatarajia kupata watalii 300 kuanzia Mei mwaka huu, katika kundi litakaokuwa la watu maarufu kutoka nchini China wakiwamo waandishi wa habari wakubwa, wafanyabiashara wakubwa na wasanii mbalimbali, pamoja na watalii 260 kila wiki mpaka hapo watakapokamilika watalii 10,000.
Naye, Meneja mauzo na usambazaji wa ATCL, Edward Mkwabi anasema shirika hilo limejipanga kufanya kazi ya kubeba watalii na makubaliano ni ya kuanza awamu ya kwanza ya kuingia kwenye mawasiliano ya namna gani biashara itakavyofanyika.
Mwenyekiti wa Kampuni ya TIHG, He Liehu anasema kampuni hiyo pia imejipanga kufanya biashara ya kuleta watalii nchini kupitia ndege zake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |