NA VICTOR ONYANGO
BEIJING, CHINA
Kama wewe ni mwanaafrika mashariki, unaposkia jina 'Sanya' unafikiria tendo la kuweka vitu tofauti pamoja ilhali kwa wachina, inamaanisha mji wenye sifa mbali mbali ikiwemo hewa safi kuliko mji wa Beijing.
Ni mji unayopatikana kusini mwa kisiwa cha Hainan kilicho kusini mwa Uchina. Mji huo unapatikana kiasi cha kilomita 2,500 na unakaa kwa ndege masaa matatu na dakika arubaini na tano.
Kwa kunyoosha pana pande wa magharibi ni nchi kama Thailand, Vietnam na Laos. Nmekuwa hapa kwa minajili ya kongamana wa nchi za Asia china ya Boao, kulingana na mtazamo wangu, mji huu umekimya sana unaezadhani shughuli za kawaida haziendelei kama kawaida.
Ukiwa unatoka Kenya ama Tanzania, chenye unawaza ni maisha ya Mombasa ama Arusha juu joto ni jingi na miti ya mnazi kila pahali.
Idadi ya watu huku ni 750,000 na kulingana na kumbukumbu za serikali, mji huu una watu wa Zaidi ya laki moja wanao miaka mia moja kuendelea. Wenye ni wavuvi, wakulima wa mchele, kahawa na mahindi na haya yote yamechanganywa na utalii wa kisasa.
Macho yangu yanavutiwa na majumba makuu yanayong'ara (skyscrapers), mwelekezi wangu ananijulisha kuwa mji wa Sanya una vyumba vya kulala laki moja na kwa usiku mmoja, mji huo unaezakubeba watalii laki mbili.
"Mji wa Sanya una uwezo wa kubeba wageni laki mbili kwa siku moja, hiyo ndiyo maana utalii umeimarika huku sana," anieleza mtafiti Tang Sixian kutoka bodi la utalii wa Sanya.
Bwana Tang ananipiga na mshangao anaponieleza kuwa tangu mwaka wa 1990 wakati mji wa Sanya ulitangazwa kuwa mji wa kiutalii wa kimataifa, hakuna mwaafrika mtalii amewahitembelea mji huo hata kama unapokea watalii zaidi ya millioni ishirini kila mwaka.
Bwana Tang anatumai kuwa baada ya sheria ya uwekezaji wa nchi za nje kupitishwa mwezi jana na National People's Congress (NPC), Afrika utatumia nafasi huo kuanza mwaka kesho kutembelea mji wa Sanya kiutalii na kibiashara.
Utalii wake umejulikana sana katika nchi 56 za Uropa, nchi hizo ziko na ndege ya moja kwa moja hadi kiwanja cha ndege wa kimataifa cha Sanya Phoenix.
Mji wa Sanya umeandaa mashindani nane ya mwanadada mrembo zaidi ulimwenguni (Miss World) na mwaka jana ulikuwa wa nane.
Wenyeji wa Sanya si wachina halisi, wanajulikana kama Li, Miao, Hui, Han na Zhuang. Watalii kutoka sehemu tofauti tofauti ya Uchina na nje wanakusanyika huku ili kuburudishwa na hali ya hewa ya kitropiki na tamaduni za Li na Miao wanaoishi kwenye kijiji kijulikanayo kama Zhongliao wakiwa na nyumba zilizojengwa kama meli. Wana Li na Miao wanatumbuiza wageni hadi na aina mbali mbali za nyimbo wakitumia firimbi (nose flute).
Kwenye hifadhi wa wanyama pori unaojulikana kama Sanya Paddy Field National Park, hapa napata mashamba makuu ya mchele wa kisasa (hybrid) na mfamo makuu wa mnyama ajulikanye kama dinosaur.
Hapa naambiwa kuwa mchele unayopatika hapa unaitwa Yuan, ulipewa jina hilo baada ya mvumbuzi wa aina hiyo wa mchele Yuan Longping mwaka wa 1954. Mchele huo unavunwa mara tatu kwa mwaka.
Nabana virago vyangu ili nirudi mji wa Beijing na kabla wa kuanza safari, napitia Xinglong coffee valley unaojulikana Uchina mzima kwa sifa yake ya kulima kahawa aina ya Robust bila kutumia mbolea ya kisasa. Huku naelewa na naibu meneja kuwa watalii wengi wanajaa huku kwa sababu ya kahawa iliyokuwa na ladha ya asili.
Kabla ya kufika uwanja wa ndege kimatifa wa Sanya Phoenix, mwelekezi wangu ananieleza kuwa tunapitia chuo kikuu cha Hainan Tropical Ocean na hapa napatana na wanafunzi arubaini na tatu kutoka nchi za Cape Verde, Comoros na Zimbabwe.
Wananieleza kuwa wamekuwa huku kwa miaka mine na wa shahada tofauti tofauti ikiwemo Utalii na kilicho ni furaisha ni kuwa wanalimiwa karo yote na serikali ya nchi ya uchina.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |