• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaihakikishia China mazingira bora ya uwekezaji, biashara

    (GMT+08:00) 2019-04-18 10:11:09

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    SERIKALI ya Tanzania imewahakikishia wawekezaji kutoka nchini China kwamba itaendelea kufanyia maboresho sera na sheria mbalimbali ambazo zinaonekana kuwa kikwazo katika shughuli mbalimbali za uwekezaji na biashara nchini humo.

    Uhakika huo umetolewa jana, Jumatano, Aprili 17 jijini Dar es Salaam, Tanzania, katika halfa ya majadiliano kati ya viongozi mbalimbali wa serikali na baadhi ya wawekezaji kutoka nchini China.

    Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji nchini Tanzania, Bi. Angellah Kairuki alisema kuwa kama nchi, wanaendelea kufanya maboresho kwenye sheria na taratibu za uwekezaji ili kila mwekezaji aweze kutambua haki na wajibu wake huku serikali ikiendelea kulinda na kuwajengea Mazingira mazuri ya kufanya biashara.

    "Katika kipindi hiki, tunahakikisha kuwa matakwa ya kisheria yanasimamiwa kikamilifu na serikali ikiwa kama mwakilishi wa wananchi inaangalia namna ya kufanya maboresho ya sera mbalimbali kwa lengo la kuweka mazingira bora na rafiki zaidi," alisema Bi. Kairuki.

    Aliwaambia wawakilishi hao wa China kuwa kwa Kushirikiana na wadau mbalimbali, wamenza kufanyia kazi mpango kazi maalum ambao utasaidia katika kuwianisha taratibu za kutoa leseni, ulipaji wa kodi na ushuru na kupunguza urasimu usio kuwa wa lazima katika sekta ya uwekezaji.

    "Napenda kushauri kwamba wakati wowote, popote, tatizo lolote linapojitokeza tusisite kutafuta ufumbuzi kwa mamlaka husika kwa njia ya majadiliano ambayo mwisho wa siku utakuwa na faida kwa pande zote mbili," alisisitiza.

    Aliwataka wawekezaji wa China ambao kwa sasa kwa mujibu wa takwimu zilizopo, ndio wanaongoza kwa uwekezaji mkubwa nchini Tanzania, kuwa tayari kuendana na mabadiliko mapya ya sera ambayo kimsingi yanalenga kurahisisha ufanyaji wa biashara na uwekezaji katika nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki.

    Alisema kuwa ili kuendelea kuvutia wawekezaji kutoka China na kwingineko duniani, serikali ya Tanzania inashugulia vikwazo mbalimbali ikiwemo ucheleweshwaji wa vibali na kufuta ushuru na kodi zisizoendana na hali halisi

    "Tutandelea kufanyia kazi maeneo mbalimbali na kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini Tanzania kwa kutatua changamoto zilizopo katika utoaji wa vibali vya kazi na makazi," alisisitiza Bi. Kairuki.

    Hivi karibuni, Waziri Kairuki alisema Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), ilianza mchakato wa kupunguza baadhi ya kodi huku Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) na wizara ya Kilimo pia tayari zimefuta baadhi ya tozo na ushuru zilizokuwa kikwazo kwa wawekezaji.

    Waziri Kairuki aliongeza kuwa serikali ya Tanzania tayari imeweka utaratibu wa kukutana na wawekekezaji mara kwa mara ili kujadiliana namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza.

    Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alisema kuwa Tanzania inaangalia namna bora ya kutumia diplomasia ya kiuchumi kuvutia wawekezaji wengi zaidi nchini.

    "Tumeanza tayari majadiliano na kutekeleza hii dhana ya diplomasia ya Kiuchumi na nchi ya China ambayo hadi sasa inaongoza kwa wawekezaji nchini. Uhusiano mzuri tulionao muda mrefu pia hutupa nafsi ya kuendelea kuboresha biashara na uwekezaji kati ya pande hizi mbili," alisema Dkt. Ndumbaro.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako