Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM
UHUSIANO wa China na Tanzania kiuchumi na kidplomasia unazidi kukua kila mwaka kutokana na mwaka jana biashara baina ya China na Tanzania kufikia dola za Marekani bilioni 3.976 ikiwa ni ukuaji kwa asilimia 15.
Katika kuhakikisha mwaka huu, biashara zinakua zaidi kampuni za China na Tanzania wameweka mikakati kuhakikisha biashara ya Muhogo China inaongeza biashara mwaka huu.
Mwaka jana uwekezaji wa jumla toka China umefikia dola za Marekani Bilioni saba na kufanya nchi hiyo kuendelea kuongoza kwa uwekezaji nchini kwa kuwa na kampuni 200 zilizowekeza na kutoa huduma nchini hadi sasa,ambazo wawakilishi wake walipata nafasi ya kuhudhuria mkutano huo.
Hayo yamebainika wakati wa mkutano wa kujadili mazingira ya uwekezaji baina ya Tanzania na China ,ulioandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji,ambapo China imekuwa nchi ya kwanza kufanya majadiliano na serikali pamoja na watendaji wakuu zaidi ya 50 wa idara na taasisi za umma kueleza namna ya kukabiliana na changamoto kwa wawekezaji.
Balozi wa China nchini Tanzania, Bibi Wang Ke amesema mikataba mpya ambayo serikali imesaini na China mwaka jana imefikia Dola za Marekani bilioni 1.3 katika miradi ya miundombinu, madini, kilimo na Viwanda, hoteli, nyumba na sekta ya fedha.
Amesema jitihada hizo zimezesha ukuaji wa uchumi, kutengeneza ajira na kuboresha maisha ya watanzania, huku akibainisha kuwa hivi karibuni wanatarajia idadi ya watalii toka Tanzania kuongezeka baada ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuanza safari zake moja kwa moja mpaka China juni mwaka huu.
Amesema kuna changamoto kadhaa katika mahusiano ya China na Tanzania yanayohitaji kufanyiwa kazi ikiwa ni pamoja na nyenzo cha ushirikiano kuangaliwa upya, kuongeza maeneo ya ushirikiano, pamoja na kuangaliwa upya masuala ya Kodi, Uhamiaji na uwekezaji.
"Katika miaka ya hivi karibuni, mazingira ya uwekezaji yamekuwa yakiimarishwa siku hadi siku, hivyo tunaamini mkutano wa leo utasaidia kumaliza changamoto nyingine zisizo za kisera huku wawekezaji wakipata maelezo halisi kutoka kwa wakuu wa taasisi za serikali waliopo" alisema.
Anabainisha kuwa ili nchi zote ziweze kunufaika na ushirikiano uliopo alitoa mapendekezo yake ikiwemo kuimarisha utekelezaji wa masuala ya maendeleo kwa kuhusisha malengo ya maendeleo ya nchi na utekelezaji wa mkutano wa ushirikiano baina ya China na Afrika (FOCAC).
Akifungua mkutano huo, Waziri wa nchi katika ofisi ya waziri Mkuu anayesimamia uwekezaji, Angella Kairuki anasema Tanzania iko tayari kusaidia wawekezaji toka China kwa lengo la kukuza uchumi kwani ni kati ya nchi chache za Afrika zinazofaidika na uwekezaji toka China.
Anaeleza kuwa katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mabadiliko ya sera mbalimbali ili kujenga mazingira bora ya uwekezaji nchini kutokana na kuwa na rasilimali za kutosha za viwanda, madini ya aina mbalimbali, hekta milioni 43 za ardhi huku hekta milioni moja zikifaa kwa kilimo cha umwagiliaji huku kukiwa na nguvu kazi ya kutosha.
Kairuki anasema mkutano huo ni wa kwanza katika kuangalia changamoto za uwekezaji katika nchi mbalimbali na tayari amekutana na mabalozi nane kwa nchi mbalimbali kuangalia namana ya kuangaa mikutano hiyo.
Amesema katika mikutano hiyo watahusisha wawekezaji wa ndani wazawa kwani mwaka pekee miradi ilioyosajiliwa TIC ni asilimia 78 na toka nje ni asilimia 28 pekee hivyo kuwezesha zaidi wawekezaji wa ndani wawekeze zaidi ikiwemo kwenda mikoani kuhamaishaha wawekezaji.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |