TANZANIA na China zimeadhimisha miaka 55 ya ushirikiano wa kidiplomasia na kuhakikisha kuendeleza ushirikiano katika nyanja mbalimbali kwa manufaa ya nchi hizo mbili.
China ni kati ya nchi za kwanza kuanza uhusiano wa kidplomasia na Tanzania mara tu baada ya kupata uhuru April 26, mwaka huu.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Maktaba mpya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambao umejengwa kwa ufadhili wa China.
Balozi wa China nchi Wang Ke anaanza maadhimisho hayo kwa kusoma salamu za Waziri wa mambo ya nje China, Wang Yi salamu za pongezi na kutaka ushirikiano huo uendelee kudumu kwa mafanikio ya pande zote.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Joyce Ndalichako aliongozana na Waziri wa Katiba na Sheria, Augustino Mahiga na Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda na viongozi wengine serikalini huku burudani mbalimbali zikitolewa na vikundi vya tamaduni ikiwemo kikundi toka China cha Shenzeni Art Company.
Waziri Ndalichako anasema urafiki huo umekuwa kwa miaka hiyo bila kuingiliana mambo ya ndani kutokana na misingi mizuri ya Rais wa Kwanza wa Tanzania Juliuss Nyerere na mwenzake wa China Mao Zedong.
Anasema katika kuimarisha uhusiano huo miongoni mwa vizazi kwenye maadhimisho kimetolewa kitabu cha uhusiano wa nchi hizo kinachoeleza mafanikio, changamoto na utatuzi uliofanywa kwa kueleza safari ya ushirikiano.
Anasema mbali na misaada mbalimbali kwa Tanzania ikiwemo Ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)kiwanda cha Khanga cha Urafiki cha ushirikiano baina ya nchi hizo, Kiwanda na Madawa cha Keko na mengineyo waliyojenga kwa nyakati za awali mpaka sasa wamekuwa misaada kwa kujenge Taasisi ya moyo Muhimbili, Kituo cha Mikutano cha Mwalimu Nyerere, Maktaba kubwa Afrika ya UDSM.
Pia, kuna shamba la mpunga mbalali,uwanja wa mpira wa Amani Zanzibar,Uwanja ya Mpira wa Taifa,mradi wa maji Chlinze na Dakawa na mengineyo. Ameeleza kuwa katika ushirikiano wa miaka 55 kwenye sekta ya elimu China imekuwa ikitoa mafunzo ya wananfunzi 100 kila mwaka lakini wameongeza kila mwaka kwa fani ya udaktari kwa miaka mitatu kuanzia mwaka jana kwa magonjwa makubw aili kupunguza rufaa nje ya nchi.
Pia Ndalichako anasema kuna nafasi ya madaktari na maensi 30 waliopo kazini kupata mafunzo ya aina mbalimbali, huku Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) kikionesha kuanzai 1990 mpaka Desemba mwaka jana miradi 723 inafanywa na wawekezaji toka China.
Anaeleza kuwa miradi hiyo imetengeneza ajira 87126huku idadi ya wawekezaji toka China ikiongezeka tangu mwaka 2011 huku mwingiliano wa raia wan chi hizo ukifanya lugha kufundishwa kwa kasi ambapo shule 15 za Sekondari nchini zinafundisha Lugha ya Kichina.
"Hii ni sehemu ndogo ya mafanikio ya ushirikiano baina ya nchi yetu na China lakini kuna mambo mengi kama ilivyoelezwa na Balozi wa China nchini ikiwemo kuletwa madaktari toka China kila mara kutoa matibabu kwa watanzania na mengineyo hivyo, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano kwa nchi hizo"alisema.
Naye Balozi Ke ,alisema China kwa miaka mitatu imekuwa ikiongoza kwa uwekezaji nchini kwa uwekezaji wa Dola za Marekani bilioni saba huku wakitoa ufadhili wa zaidi ya 1700 na zaidi ya fursa za mafunzo 6000 nchini na mengineyo.
Alisema kuna sababu tatu za mafanikio ya ushirikiano wa China na Tanzania kwa kuheshimiana,kuweka urafiki kwanza kwa mafanikio ya nchi hizo na kuwa na ushirikiano wenye manufaa kwa wote.
Alisema katika mkutano wa pili wa Ushirikiano wa Kiamtaiafa wa Njia moja ukanda mmoja (BRF) unaoendelea Beijing China Unahusisha washiriki 5,000 kutoka nchi zaidi ya 150 na taasisi za kimataifa 90 huku Tanzania ikiwakilishwa na Rasi Mstaafu Jakaya Kikwete na Waziri wa Kazi, Usafiri na Mawasiliano Isack Kamwele kwa kutarajia mengi katika kuimarisha uhusiano wan chi hizo mbili katika BRT.
"Pia, naomba kutangaza kuwa Tanzania pia itashiriki kama wageni rasmi katika Maonesho ya biashara ya kwanza kati ya China na Afrika yatakayofanyika Juni mwaka huuhuku ikialikwa maonesho ya pili ya kimataifa ya China kwa wafanyabiashara wa bidhaa za ndani na nje ya nchi hiyoutakaofanyika Novemba mwaka huu" alisema.
Balozi alisema matukio hayo mawiali ya uchumi na biashara itawezesha Tanzania kuonesha bidhaa zake hivyo kukuza ushirikiano wa kibiashara hususan Tanzania kuuza bidhaa Chinaambapo China inahamasisha Kampunizake kuwekeza Tanzania na kusaidia maendeleo ya uchumi na kijamii.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |