• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu China wakamata ajira zaidi ya 100,000 EAC, Tanzania, Kenya zaongoza

    (GMT+08:00) 2019-05-05 08:56:40

    Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    NCHI za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekuwa fursa kubwa ya ajira kwa wataalamu wa taifa la China, baada ya kutoa ajira zaidi ya 123,524. Ajira hizo ni kupitia kandarasi za miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara, viwanda na nishati.

    Taarifa za Kitabu cha Mwaka cha Takwimu cha China na Shirika la Takwimu la Taifa la China, Kenya ndiyo inayoongoza kwa kutoa ajira nyingi kwa wachina baada ya kuajiri watalaamu 40,113.

    Aidha, vyanzo hivyo vya habari vimeonesha kuwa Tanzania imeshika nafasi ya pili baada ya kutoa ajira kwa wananchi wa China 39,614 katika miradi mbalimbali katika sekta ya miundombinu ya barabara na viwanda.

    Takwimu hizo zimeonesha kuwa Uganda imefanikiwa kutoa ajira kwa Wachina 24,044, hivyo kuifanya kushika nafasi ya tatu katika nchi za EAC ikiwa katika nafasi ya tatu. Katika taifa hilo ambalo ni la tatu kwa ukubwa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Wachina wameajiriwa katika sekta za miundombinu ya barabara, mawasiliano, Tehama na sekta ya nishati.

    Rwanda imeshika nafasi ya nne kwa kutoa ajira kwa wachina ambapo imewaajiri wapatao 8,301 katika sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, teknolojia na nishati.

    Taarifa hizo zimeonesha kuwa Sudan Kusini pamoja na kwamba imejipatia Uhuru wake miaka nane iliyopita imeshika nafasi ya tano kwa kuwavutia wawekezaji wa China na nchi ina Wachina 7,863 walioajiriwa n katika sekta za miundombinu na nishati.

    Burundi imeshika nafasi ya mwisho kwa kuwavutia wawekezaji wa Kichina ambapo imefanikiwa kuwavutia wawekezaji hao kiasi cha 3,589 katika kipindi cha kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2017.

    Hii inaonesha kuwa China imevutiwa kwa kiasi kikubwa katika jumuiya ya Afrika Mashariki katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Kutokana na uwekezaji huo kampuni mbalimbali za China zimeweza kuingiza fedha za kutosha katika nchi za Afrika Mashariki.

    Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini China, Kenya ndio inayoongoza kwa kuziingizia fedha nyingi kampuni za Kichina kutokana na uwekezaji wao nchini humo.

    Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, kampuni mbalimbali ya Kichina zimevuna kiasi cha dola za Marekani bilioni 20 wakati kampuni ya Kichina zilizowekeza Tanzania zimefanikiwa kupata dola za Marekani bilioni 12.7 katika kipindi kama hicho.

    Uganda imeshika nafasi ya tatu kwa kuziingizia kampuni za China fedha nyingi kutokana na uwekezaji wao nchini humo. Taarifa zimeionesha Uganda kuwa imeingiza kiasi cha dola za Marekani bilioni 8.7 kwa kampuni za China yalizowekeza nchini humo.

    Kwa upande wa mikopo, China imekuwa ikimimina fedha za mikopo kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 hadi 2017, Kenya imepokea kiasi cha dola za Marekani bilioni 9.8.

    Katika kipindi hicho, Uganda ilipokea kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.9, Tanzania ilipokea kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.3 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.

    Ukiachilia mbali nchi za EAC, China imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa nchi za Afrika, kiasi cha kuanzishwa ushirikiano unaokutanisha Serikali ya China na mataifa karibu yote ya Afrika kila mwaka kupitia mkutano wa ushirikiano wa China Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako