Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam
Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania, wanafunzi wa kidato cha nne wanaosoma lugha ya Kichina mwaka huu wataanza kufanya mtihani wa somo hilo katika mitihani yao ya taifa.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Prof. Aldin Mutembei, taratibu zote zimeshafanyika na wameshajiandaa kutekeleza mpango huo.
Alisema Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Tanzania tayari imeshapitisha mpango huo uliolenga kuhakikisha kuwa wanafunzi hao wanafanya somo hilo katika mitihani yao ya mwisho.
"Kwa mara ya kwanza wanafunzi wa kidato cha nne wanaosoma lugha hiyo nchini watafanya mtihani wa somo hilo," alisema mkuu wa Taasisi hiyo.
Prof Mutembei alibainisha hayo katika hafla ya kufungua rasmi programu ya walimu wa Kichina waliopo katika nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki kufundisha lugha hiyo. Hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Prof Mutembei alisema hadi sasa, nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki ina vituo 22 ambapo lugha hiyo ya Kichina hufundishwa.
Alitaja vituo hivyo kuwa ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma na pia katika baadhi ya shule za sekondari na msingi nchini.
Alisema mwaka jana, baadhi ya wanafunzi wa kidato cha pili walifanya mtihani wa somo hilo katika mitihani yao ya taifa na mwaka huu pia somo hilo litaendelea kufanywa.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof Bonaventure Rutinwa alisema kuwepo kwa Taasisi ya Confucius chuoni hapo kumewezesha wanafunzi wanaosoma programu hiyo kuwa na uwelewa mpana juu ya mambo ya utamaduni na mchango wake katika maendeleo ya jamii.
"Wanafunzi wetu wanavyosoma somo hili la lugha ya Kichina kumewapa uelewa mpana namna utamaduni ulivyo na faida kubwa katika maendeleo ya jamii. Fursa hii pia huwawezesha kuelewa ushirikiano wa hizi nchi mbili katika mambo
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo pia aliwataka walimu hao kutoka China kujikita katika kubadilisha uzoefu na kushauri namna bora ya kuhumarisha na kuboresha ufundishwaji wa somo hilo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |