• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Upembuzi yakinifu chuo kinachofadhiliwa na China wakamilika

    (GMT+08:00) 2019-06-12 09:31:33

    Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    UPEMBUZI yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa Chuo kikuu cha Usafirishaji nchini Tanzania utakaofadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Watu wa China, umekamilika.

    Chuo hicho ambacho kitarajiwa kujengwa jijini Dar es Salaam na kuwa kati ya moja ya vyuo vikubwa barani Afrika kitagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 130 za Tanzania.

    Mkuu wa Chuo Cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa amesema kuwa upembuzi yanikifu kwa ajili ya mradi huo ulikamilika mwezi Machi mwaka huu.

    Aliweka bayana kuwa kwa sasa kinachosubiriwa ni serikali za nchi hizo mbili --Tanzania na China kuupitisha ili ujenzi wa chuo hicho uanze mara moja.

    Alisema ujenzi wa chuo hicho unalenga, pamoja na mambo mengine, kusaidia kusukuma jitihada za serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo na kuzalisha wataalamu kwenye nyanja hiyo.

    Balozi wa China nchini, Bi. Wang Ke mwaka jana mwezi Februari alimwambia Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwamba China imeridhia kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

    Balozi Wang alieleza kuwa msaada huo ni sehemu ya misaada na miradi mbalimbali ambayo China inaitekeleza nchini Tanzania yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati yake na Tanzania.

    Mpango huo unahusisha vyuo vikuu vitano vya usafirishaji barani Afrika ambavyo vimo katika mpango wa Serikali ya China ya kujenga au kuendelezwa vyuo vya usafirishaji kwa hadhi ya chuo kikuu.

    Mwakilishi wa Serikali ya China wa masuala ya uchumi na biashara, Lin Zhiyong amewahi kutembelea eneo la mradi huo ambalo ni chuo cha NIT kilichopo Mabibo, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

    Alisema ujenzi wa majengo mapya katika chuo hicho unatarajia kuanza muda si mrefu na ni utekelezaji wa ahadi ya Rais wa China, Xi Jinping, aliyoitoa akiwa Afrika Kusini mwaka 2015.

    Alisema licha ya ushindani wa kupata nafasi hiyo, Tanzania itapewa kipaumbele cha kwanza kwa sababu ya urafiki wa muda mrefu baina yake na China.

    "Tumefurahi kuona jitihada zinazofanywa na NIT pamoja na mpango wa upanuzi wa chuo hiki, hivyo napenda kuwahakikishia kwamba Tanzania itapewa kipaumbele cha kwanza kati ya vyuo vitano vya usafirishaji vitakavyojengwa barani Afrika miaka mitatu ijayo.

    "Kilichobaki ni chuo kiandae andiko la mradi huo na kililete katika ubalozi wetu, tutapitia na kuwapa utaratibu mwingine wa kufanya ili wataalamu wetu waje waanze ujenzi," alisema Zhiyong.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako