• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yawanusuru tembo wawili Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-07-03 09:07:45

    Na Majaliwa Christopher

    KAMPUNI ya ujenzi ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) imesaidia kuokoa tembo wawili waliokwama katika matope kwa siku mbili katika eneo la Itigi Mkoani Singida, Tanzania.

    Afisa kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Bw. Peter Marcely, alithibitisha kuwa tukio hilo lilitokea mwezi Juni, 22 katika kijiji cha Doroto iliyopo katika kata ya Itigi.

    Bw. Marcely alisema kwamba tembo hao wawili walikwama katika matope hayo baada ya kutoka katika hifadhi ya Muhesi ili kutafuta maji kwenye maeneo ya jirani.

    Alisema kuwa baada ya kazi hiyo ya kuwaokoa tembo hao kuonekana kuwa ngumu, maafisa wa TAWA waliamua kuomba msaada kutoka kwa kampuni hiyo ya China wanaofanya kazi ya ukarabati wa reli ya kati.

    "Kazi ya kuwaokoa tembo hao ilihitaji mashine makubwa kama tingatinga. Njia pekee ilikuwa ni kutafuta msaada kutoka kwa wenzetu wa China walioweka kambi takribani kilomita 80 kutoka kwenye eneo la tukio," alisema.

    Aliongeza kuwa kazi hiyo ilitekelezwa na wataalamu wa TAWA wakishirikiana na mainjinia kutoka katoka kampuni hiyo ya China.

    Mwaka 2017, Kampuni ya ujenzi ya China Sinohydro iliwapeleka wahandisi wake na tingatinga katika eneo la kuhifadhi wanyama pori la Rungwe katikati ya Tanzania ili kuwaokoa tembo watano waliokwama katika shimo.

    Katika tukio hilo, tembo wanne wakiwemo watoto wawili waliokolewa lakini mmoja mkubwa alikufa kutokana na ukosefu wa maji.

    Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo ya CCECC, ilisema kwamba baada ya kuombwa msaada na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, walitoa timu ya wataalamu pamoja na tingatinga na kufanikiwa kukamilisha zoezi hilo kwa ufanisi mkubwa.

    "Timu ya wataalamu walifika katika eneo la tukio majira ya mchana. Tuliweka mkakatati wa pamoja kwa kushirikiana na wataalam wa TAWA. Kazi hiyo tulilifanikisha na tembo hao kuondoka wakiwa hai," alisema Meneja Mradi wa kampuni hiyo ya CCECC Bw. Bai Cunxian.

    Alisema baada ya zoezi hilo muhimu, kila mtu aliekuwepo katika eneo hili alifurahi na kuusifu ushirikiano uliokwepo katika ya maafisa hao wa TAWA na wataalamu kutoka kampuni ya CCECC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako