• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni za China zazidi kushinda zabuni za miradi Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-07-04 09:34:33
    Na Majaliwa Christopher

    SERIKALI ya Tanzania imeendelea kuingia mikataba ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na kampuni za China, hatua inayoashiria ubora na ufanisi wa kampuni hizo kutoka nchi hiyo ya Asia ya Mashariki.

    Jana Jumanne, Julai 2, Kampuni ya Shanxi Construction ya China imeingia mkataba na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wa mradi wa msambazaji maji safi katika mji wa Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

    Mkataba huo ulisainiwa jijini Dar es Salaam kati ya mwakilishi wa Shanxi Construction Bw. Lio Zerong na Ofisa Mtendaji wa DAWASA Bw. Cyprian Luhemeja kwa niaba ya serikali ya Tanzania. Kwa mujibu wa Bw. Luhemeja, mradi huo wa Mkuranga utagharimu Shilingi Bilioni 5.5 za Tanzania.

    Mradi huo utahusisha ujenzi wa tenki kubwa lenye ukubwa wa kuhifadhi maji lita milioni 1.5 na kunufaisha wananchi 25,000.

    Katika hafla hiyo iliyoshuhudiwa na Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa, miradi mingine mitano ya usambazaji maji pia ilisainiwa. Miradi hiyo yote kwa ujumla inagharimi Shilingi Bilioni 114 za Tanzania.

    Miradi hiyo kwa ujumla inalenga kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Jiji la Dar es Salaam na miji katika Mkoa wa Pwani.

    Kukamilika kwa miradi hiyo kutupunguza tatizo la majisafi na salama katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.

    Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Maji Alisema miradi mitano kati ya sita iliyosainiwa jana inatekelezwa kwa fedha za ndani na mradi mmoja unatekelezwa kwa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.

    Naye Mwenyekiti wa Bodi wa DAWASA, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu, Jenerali Davis Mwamunyange, alisema miradi hiyo ikikamilika itaweza kuwanufaisha wananchi 1,870,000 wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, lakini pia itasaidia kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es Salaam kutoka asilimia 85 hadi asilimia 95.

    "Baadhi ya mapungufu ambayo yanaikabili DAWASA ni tatizo la kuwapelekea wananchi ankara zisizo sahihi pamoja na kutochukua hatua za haraka kuhusu matatizo ambayo wananchi wanayaripoti kama vile kukatika kwa mabomba au kukosekana kwa maji,"alisema Jenerali Mwamunyange.

    Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alisema kuwa Wizara imeanzisha huduma ya Wakala wa Maji Vijijini kwa lengo la kuhakikisha wananchi wa vijijini nao wanapata maji safi na salama. Alisema wahandisi wa maji ambao katika maeneo yao hakutakuwa na maji watafute kazi zingine.

    Viongozi wengine walioshuhudia utiaji saini mkataba wa miradi hiyo jana ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako