• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • DIT kuzalisha wataalamu wa Teknolojia na Ufundi kwa kushirikiana na Chuo Cha Teknolojia na Ufundi cha Nanning China

    (GMT+08:00) 2019-07-12 08:51:59

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    TANZANIA kupitia Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT) imesaini makubaliano ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali za utoaji wa elimu na Chuo cha Teknolojia na Ufundi 'Nanning' kutoka nchini China kusaidia kuzalisha wataalam wenye weledi wa kutosha katika fani zote zinazofundishwa katika taasisi hiyo.

    Mkuu wa taasisi hiyo, Profesa Preksedia Ndomba anasema ushirikiano huo ambao utajikita zaidi katika kukuza maendeleo ya kitaaluma kwa wanafunzi na wakufunzi, umekuja wakati muafaka ambapo Taifa linajipambanua katika suala zima uchumi wa viwanda.

    Alisema kutokana na hatua hiyo ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati wa viwanda ifikapo Mwaka 2025, DIT imekuwa mstari wa mbele kuzalisha wabunifu mbalimbali kwa ajili ya kulisaidia taifa kufikia malengo hayo, hatua inayokifanya kuanzisha ushirikiano na vyuo mbalimbali vya nje ya nchi ambavyo kimsingi vimepiga hatua kubwa katika eneo la teknolojia.

    "DIT ni moja wa wadau muhimu katika kufanikisha azma hiyo ya Serikali ya uchumi wa Viwanda, kwa kipindi cha miaka miwili tumeweza kuingia ushirikiano na vyuo mbalimbali vya nje, lengo ni kubadirishana uzoefu utakaotusaidia kuwapata wataalam wenye uwezo katika nyanja mbalimbali, hii itatuwezesha kujifunza mitazamo chanya na kufikia malengo tuliyojiwekea" alisema Profesa Ndomba.

    Kupitia makubaliano hayo, Profesa Ndomba alisema wanafunzi wanaosoma chuo hicho, pia wataweza kujifunza kwa vitendo mbinu mbalimbali utendaji kazi katika viwanda, sambamba na eneo la uongozi ambapo wataalam kutoka Chuo cha Naninng wamebobea kwa kiasi kikubwa .

    Naye Makamu wa Rais kutoka Chuo cha Nanning Profesa Hu Weidong, alisema kupitia ushirikiano huo wataweza kuboresha eneo la utoaji wa elimu ikihusisha miundombinu ya taasisi pamoja, vifaa vya ufundishaji pamoja na kuboresha mitaala inayoendana na matakwa ya kimataifa.

    Aliyataja maeneo mengine kuwa ni pamoja na kuhamaisha uanzishaji wa program za masomo za pamoja na ushirikiano katika kubadirishana wakufunzi, pamoja na kuwaunganisha kimafunzo wanafunzi katika taasisi zingine za kimataifa pamoja na maeneo ya viwanda.

    Taasisi ya Tekonolojia ya Dar es Salaam (DIT) yenye miaka 62 tangu kuanzishwa kwake, imekuwa mstari wa mbele katika kuzalishwa wataalam mbalimbali wanaolitumikia taifa katika maeneo ya viwanda na kwingineko na hivyo kuwa msaada mkubwa katika kukuza uchumi kupitia wataalam hao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako