• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Msumbiji, Nigeria zaiomba China kusaidia kilimo cha mpunga

    (GMT+08:00) 2019-07-19 10:07:10

    Na Deogratius Kamagi, Beijing

    Nchi za Msumbiji na Nigeria zimeiomba China kuzisaidia katika mbinu za kuboresha kilimo cha mpunga kwa ajili ya kuongeza uzalishaji na kuokoa gharama za kuagiza chakula hicho nje ya nchi.

    Wakati Msumbiji inanunua wastani wa tani 370,000 za mchele kwa mwaka kutoka nje ya nchi, Nigeria huagiza wastani wa asilimia 22 za mchele kwa ajili ya chakula kutoka nje.

    Wakizungumza katika semina maalumu ya kuhusu ushirikiano baina ya China na nchi za Afrika katika uzalishaji wa mpunga leo Jumatano, Mkurugezi wa kilimo kutoka Msumbiji Dokta Pedro Dzucula na Mkurugenzi wa kilimo kanda ya Kaskazini Magharibi wa Nigeria Mhandisi Matthew Owalabi wamesema wana imani ushirikiano uliopo baina ya nchi zao na China utaendelea kuleta tija katika sekta ya kilimo.

    Dokta Dzucula amesema, pamoja na jitihada mbalimbali ambazo nchi yake inazichukua katika kukuza zao la mpunga, bado kuna changamoto ya ukosefu wa zana za kisasa pamoja na wataalamu wa kutosha kusaidia kuongeza uzalishaji.

    "Msumbiji ina eneo lenye ukubwa wa hekta milioni 26 zinazofaa kwa kilimo lakini hadi sasa tumeweza kutumia hekta milioni 6.2 tu hivyo zaidi ya asilimia 70 ya ardhi haitumiki," alisema na kuiomba serikali ya China kusaidia kutoa mafunzo na kubadilishana uzoefu katika sekta ya hiyo.

    "Kwa kuzingatia umuhimu uliopo, ni wazi tunahitaji msukumo wa kipekee kwani Mchele ni chakula muhimu sana kwa nchi yetu" aliongeza.

    Kwa upande wake, Mhandisi Owalabi alisema nchini Naijeria, kilimo kinachangia kwa kiazi kikubwa pato la taifa na kwamba hadi kufikia mwaka 2010 sekta hiyo ilikua imeajiri asilimia 10 ya wanaijeria.

    "Lakini bado kuna haja ya kuendelea kufanya maboresho ya kimkakati katika sekta ya kilimo kwani sekta hii imekua ni mkombozi katika kuinua maisha ya wananchi hasa wa maeneo ya vijijini," alisema.

    Pia alitumia wasaa huo kutaja changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya kilimo nchini Naijeria. Changamoto hizo ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara hasa kutika maeneo ya vijijini, magonjwa, ukosefu wa masoko ya uhakika na kukosekana kwa wawekezaji sahihi.

    "Kwa hivyo tunatumia fursa hii kukaribisha wawekezaji pamoja na wabia wa maendeleo ambao kwa pamoja tunaweza kushirikiana nao katika kuleta maemdeleo ya pamoja na kila upande kunufaika kutiokana na ushirikiano huo," aliongeza.

    Awali, katika hotuba yake ya ufunguzi katika semina hiyo ambayo imeratibiwa na taasisi ya Bill & Melinda Gates, Afisa miradi mwandamizi, Liu Dong alisema wana matumaini kuwa nchi hizo zitashiriakiana na kuleta tija katika kukuza zao la mpunga hivyo kuhakikisha nchi za Afrika zinakua na chakula cha kutosha mwaka mzima.

    "Kumekua na changamoto ya chakula katika maenep mengi ya Afrika hivyo ni matarajio yetu kuwa ushirikiano huu utamaliza tatizo hilo," alisema.

    Kwa upande wake, Mkurugenzi kutoka wizara ya Biashara ya China Zhang Ning alisema taifa hilo la pili wkwa ukuaji wa uchumi duniani lipo tayari na litaendelelea kushirikiana na nchi zinazoendelea katika kuleta maendeleo na kutatia changamoto mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako