• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Xinhua, TSN wakubaliana kudumisha ushirikiano na kukuza Kiswahili

    (GMT+08:00) 2019-07-22 10:26:40

    Na Theopista Nsanzugwanko, DAR ES SALAAM

    USHIRIKIANO baina ya Vyombo vya habari China na Tanzania unazidi kushika kasi baada ya Shirika la Habari la China, Xinhua na Kampuni ya Magazeti ya Serikali Daily News, Habari Leo (TSN), zimezidi kudumisha ushirikano ikiwa ni pamoja na kuendeleza programu ya lugha ya Kiswahili kwa Wachina.

    Mhariri wa HabariLeo, Nicodemas Ikonko wakati akimkaribisha Mhariri Mkuu wa Shirika la Habari la Xinhua, He Ping walipotembelea kampuni ya TSN ikiwa ni mkakati wa kudumisha ushirikiano uliopo kati ya China na Tanzania.

    Ikonko alisema kwa kuwa China imetilia mkazo kuendeleza uhusiano wa kirafiki na nchi za Kiafrika hususani Tanzania tangu kuasisiwa kwake, TSN ipo tayari kutoa mafunzo ya kiswahili kwa Xinhua kupitia gazeti la HabariLeo na mtandao wa Tsn Online kwa ajili ya kuzidisha mwingiliano na uelewano pamoja watu China na Tanzania.

    Alisema kwa kufanya hivyo anamini kutaweza kusaidia ufundishaji wa Kiswahili kupitia gazeti katika kukuza na kueneza Kiswahili nchini China.

    Mhariri wa Gazeti la Dailynews Pudensiana Temba anasema ushirikiano wa Tanzania na China ni wa muda mrefu ulioasisiwa na baba wa mataifa yote mawili ambao ni hayati Julius Nyerere na Mao Zedong.

    Anasema uhusiano huo umekua mzuri kwa fursa mbalimbali za maendeleo kwa pande zote mbili ambapo katika sekta ya habari TSN imekuwa ikishirikiana vyema na Xinhua pamoja na chombo kingine cha habari cha People's Daily ambapo zaidi ya waandishi 20 walishakwenda kupata mafunzo ya muda mfupi na mrefu nchini China ikiwa ni pamoja na kubadilisha uzoefu.

    Aidha Temba anaushukuru pia ubalozi wa China nchini Tanzania ambao umekuwa ukitoa udhamini wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Tanzania.

    Naye, Mhariri Mkuu wa Xinhua He Ping anasema ni mara ya kwanza kutembelea TSN na kuahidi kudumisha uhusiano uliopo kwa kuwa vyombo vyote viwili vinamilikiwa na serikali na pia ni vyombo vikubwa kwenye nchi zote mbili.

    Anasema kwa sasa Xinhua inapatikana katika nchi 23 duniani Tanzania ikiwemo na kuhaidi kuipa ushirikiano TSN ili iweze kupiga hatua katika sekta ya habari.

    Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN Baraka Katemba alisema ujio huo wa He Ping na jopo lake utasaidia kukuza taaluma ya habari kwa pande zote mbili kwa kuwa lengo la ujio wao ni kukuza mahusiano kati ya China na Tanzania katika masuala ya vyombo vya habari .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako