• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China yasaini mkataba kuongeza watalii na uwekezaji Zanzibar

    (GMT+08:00) 2019-07-23 09:39:06

    Na Theopista Nsanzugwanko, ZANZIBAR

    WIZARA ya habari Utalii na Mambo ya kale imetiliana saini makubaliano ya kuimarisha uhusiano katika sekta ya utalii na kampuni ya kimataifa ya touchroad kutoka jimbo la Zhejiang ya China yenye lengo la kuongeza idadi ya wa watalii wanaokuja zanzibar kutoka nchi hiyo.

    Makubaliano hayo yalitiwa saini na Katibu mkuu wizara habari utalii na mambo ya kale Khadija Bakari Juma na mwenyekiti wa kampuni ya touchroad he lie hui katika hoteli ya park hyatt shangani mjini zanzibar.

    Katibu mkuu Khadija Bakari alisema lengo ni kuweka miundombinu bora itakayovutia watalii ikiwemo kuwepo usafiri wa ndege ya moja kwa moja kutoka china hadi Zanzibar.

    Alisema wamekubaliana zanzibar kuongeza matangazo ya vivutio vya utalii vilivyopo nchini katika vyombo na taasisi zinazoshughulikia utalii za china kwa kutumia lugha ya kichina ili wananachi wengi wapate nafasi ya kuvielewa.

    Alieleza matarajio yake kwamba kutokana na histori ya zanzibar na vivutio viliopo iwapo vivutio viliopo zanzibar vitatangazwa kikamilifu idadi ya watalii kutoka nchi hiyo itakua kwa haraka.

    Akizungumza katika jukwaa hilo, katibu mkuu wizara biashara viwanda na masoko Juma reli aliyataja maeneo mengine waliokubaliana katika mkataba huo ni kuanzisha uwekezaji wa viwanda kwa wafanyabiashara wa wakubwa wa china kuja kuwekeza zanzibar.

    Alisema kupitia makubaliano hayo wananchi wa zanzibar wataendelea kunufaika kupitia sekta ya utalii hivyo amewaomba kuchangamkia fursa zinazotokana na utalii kwa kuwa wabunifu ili kuweza kuongeza kipato chao.

    Naye, Mkurugenzi masoko kamisheni ya utalii zanzibar Dr Miraji Ukuti amesema kufuatia makubaliano hayo ndani ya mwaka huu kiasi cha watalii 3000 kutoka china wataingia Zanzibar na idadi hiyo itaongeza kufikia watalii 7000 katika mwaka unaofuata.

    Akizungumzia utamaduni wa vyakula vya mataifa mbali mbali katika hoteli Zanzibar Dr. Miraji alisema amesema kwa sasa zipo vizuri katika kupika mapishi ya mataifa mbali mbali ikiwemo mapishi ya kichina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako