• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya China kukamilisha ujenzi stendi ya mabasi ya kimataifa Tanzania mwaka 2021

    (GMT+08:00) 2019-07-24 10:18:40

    Na Majaliwa Christopher, Dar es Salaam

    MRADI wa ujenzi wa stendi ya mabasi ya kimataifa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro, Kaskazini mwa Tanzania, unaotekelezwa na kampuni ya China Railway Jianchang Engineering (CRJE) unatarajiwa kukamilika Januari mwaka 2021.

    Kampuni hiyo ya China inatekekeleza mradi huo kwa kushirikiana na makanadarasi wasaidizi watano kwa gharama ya Shililingi Bilioni 28.8 za Tanzania, na kukamilika kwake kunategemea kuchochoea shughuli mbalimbali za maendeleo na uwekezaji katika mikoa ya Kaskazini mwa nchi hiyo ya Afrika ya Mashariki.

    Akiwa Mkoani Kilimanajaro, akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo mkubwa wa mabilioni ya shilingi, Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alisema mradi huo ni maalum na wa kimkakati kwani uko miongoni mwa miradi ambayo Serikali ya Tanzania imekuwa ikiweka utaratibu wa kupelekea fedha kwenye miradi iliyotengwa na halmashauri.

    "Serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi huu…ujenzi wa stendi hii unatarajiwa kukamilika Januari 2021 na unafanywa na mkandarasi mkuu ambayo ni kampuni ya CRJE ya China ikishirikiana na makandarasi wasaidizi watano," alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

    Stendi hiyo itakayokuwa na ofisi, maduka, migahawa na hoteli, itakuwa na uwezo wa kuhudumia mabasi 300 kwa siku ambayo yataingia na kutoka ambapo kati ya mabasi hayo 72 yanaweza kuegeshwa kwa wakati mmoja. Pia kutakuwa na maegesho ya ya magari binafsi 218, teksi 34 na bajaji na bodaboda 20.

    Waziri Mkuu Majaliwa aliongeza kuwa mradi huo umelenga kuondoa msongamano wa mabasi katikati ya mji wa Moshi lakini pia kuongeza mapato ya Manispaa.

    "Baadaye hapa mtaboresha biashara zenu, kukamilika kwa stendi hii, biashara ya teksi, daladala na bodaboda zitafanyakazi kubwa, hatutaki mipango hii ikwame," alisema

    Serikali kupitia Manispaa ya Moshi mkoani kilimanjaro, ulisaini mkataba wa ujenzi wa kituo kipya cha kimataifa cha mabasi Ngangamfumuni na kampuni ya ya CRJE (East Africa) Ltd ya China mwezi Januri mwaka huu, 2019.

    Ujenzi wa kituo hicho cha mabasi umeanza rasmi Januari 28 mwaka huu na utadumu kwa miezi 24 na unatekelezwa na kampuni ya ukandarasi ya CRJE ya nchini China ambayo imeahidi kukamilisha kwa wakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako