Na Theopista Nsanzugwanko
KIWANDA cha kutengeneza vigae "Tiles" nchini cha Goodwill Tanzania Ceramic Limited kilichopo katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani,kinachomilikiwa na mwekezaji toka China kimeshika soko katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Kiwanda hicho kinachotumia gesi asilimia kuzalisha bidhaa zake tangu kuanzishwa kinasafirisha tani 300 kwa mwezi kwenda nchi za Rwanda Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) huku tani hizo 300 zikisafirishwa kwa wiki kuingia Nairobi Kenya. Pamoja na nchini Tanzania wakiuza tani 300 kwa wiki.
Meneja Uendeshaji wa kiwanda hicho, Msafiri figa anasema tangu kuanza kwa kiwanda katika mwaka wa tatu sasa wamekuwa wakitumia gesi asilia jambo ambalo hawajawahi kusimamisha uzalishaji na kufanikiwa kutoa ajira kwa wananchi.
Anasema katika kiwanda kinachomilikiwa na Mwekezaji toka China kina uwezo wa kuzalisha futi za mraba 80,000 kwa siku lakini wamekuwa wakizalisha chini ya kiwango hicho kwa kuzalisha futi za mraba 30,000 mpaka 40,000 kutokana na kukosa soko la ndani.
Anataka serikali kuingilia kati kwa kusitisha uagizaji wa vigae hivyo nchini kwani kuna viwanda viwili vitakavyoweza kumudu mahitaji ya soko la ndani na kusafirisha nje ya nchi.
Anasema wamekuwa na changamoto ya masoko lakini katika Ukanda wa Afrika Mashariki wamekamata soko la Kenya hususan katika jiji la Nairobi kwani awali walikuwa wakisafirisha roli 30 hadi 40 kwa siku ambazo ni sawa na tani 900 hadi 1,200 kwa wiki.
Anasema kutokana na ubora wake vigae hivyo vimekuwa vikipendwa sana hususan Nairobi lakini kuna kiwanda cha kutengeneza vigae cha nchini humo lakini watu wamekuwa wakinunua za goodwii hivyo kuwepo na changamoto nyingi katika uingiza bidhaa hizo ili kulinda soko lao la ndani.
"katika eneo hili ,tunashukuru serikali kwani mara nyingi tumekuwa tukipata changamoto kubwa kwa kutuwekea vikwazo kuingiza bidhaa hii ,lakini serikali imetusaidia na tunaendelea na biashara lakini kwa kiwango kidogo tofauti na awali "alisema
Anabainisha pia kuwa mbali na Kenya kwenye soko kubwa wanapeleka nchi nyingine za Rwanda na Burundi kwa Malori matano hadi 10 kwa mwezi ambapo bado biashara haijakuwa vizuri lakini wanatarajia kuongeza usambazi wake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) James Mataragio na watendaji wake kutembelea viwanda hivyo vinavyotumia gesi asilia kuona maendeleo yake walibainisha masoko hayo kuliko soko la ndani.
Anaeleza kuwa wakiwa wameajili wanazalisha tani 400 kwa siku ambayo ni sawa na tani 10,000 kwa mwezi hivyo kutafuta masoko ya ndani nan chi nyingine za ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati akihitimisha ziara hiyo, Mataragio anasema TPDC imepanga kuongeza idadi ya viwanda vinavyotumia gesi asilia nchini ndani ya miaka mitatu kwa kuunganisha Viwanda 10 hivyo kufanya Viwanda 54 kutumia gesi asilia hivyo kupunguza gharama za uzalishaji.
Kwa sasa Viwanda 44 vinatumia gesi asilia ambayo ni nishati ya gharama nafuu kwa kuokoa gharama ya matumizi kwa asilimia 50 hivyo uzalishaji bidhaa kuwa nafuu na wananchi kupata kwa urahisi na gharama nafuu.
Mataragio na watendaji wakuu wa shirika hilo walitembelea Viwanda vitatu vya Goodwill kinachozalisha vigae (Tiles) kinachotumia gesi kwa miaka mitatu, kiwanda cha Lodhia still kinachotengeneza nondo kinachotumia gesi miezi miwili, pamoja kiwanda cha Knauf kinachotengeneza jasi kinachoendelea na ujenzi wa miundombinu ya kuingiza gesi kiwanda hapo.
Mataragio anasema baada ya kutembelea Viwanda hivyo na kuona miundombinu ya gesi asilia wawekezaji wamefurahi kuokoa gharama kwa kutumia gesi asilia na kuwaalika wawekezaji zaidi kuunganisha na gesi kwa miundombinu ipo tayari na Kuna gesi ya kutosha.
Anasema Viwanda 44 vinavyotumia gesi vipo mikoa ya Mtwara, Dar es Salaam na Pwani huku Viwanda vingine vikiwa katika hatua mbalimbali za kuingiziwa gesi hivyo wamejiwekea lengo katika miaka mitatu ijayo kuunganishia viwanda 10 zaidi.
Anasema viwanda hivyo 44 wanatumia gesi za mita za ujazo takribani milioni 39 ambazo ni kiasi kidogo hivyo kutaka viwanda zaidi kujitokeza kutumia gesi kwani licha ya kuwa gharama nafuu ni rafiki wa mazingira.
"Bei zetu tunazotumia viwandani ni elekezi kulingana na Ewura ambayo ni nafuu ukilinganisha na gesi za kwenye mitungi au mafuta mazito kwa chini ya asilimia hamsini" alisema.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |