• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waandishi wa habari Zanzibar Waadhimisha miaka 70 ya Taifa la China

    (GMT+08:00) 2019-08-19 10:34:27

    Na Majaliwa Christopher

    SERIKALI ya Jamhuri ya Watu wa China itaendelea kushirikiana na Tanzania na nchi zingine za Afrika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta za afya, miundombinu, elimu, maji na rasilimali watu.

    Hayo yalisemwa na Balozi Mdogo wa China aliepo Zanzibar Xie Xiaowu katika sherehe za miaka 70 ya kuundwa kwa Jamuhuri ya Watu wa China na miaka 55 ya uhusiano wa Kidiplomasia kati ya China na Tanzania.

    Sherehe hizo zilifanyika visiwani Zanzibar na kukutanisha waandishi wa vyombo vya habari na maafisa wa ubalozi mdogo wa China visiwani humo.

    Bw. Xie alisema China imekuwa mshirika mkubwa wa kimaendeleo kwa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika sekta mbalimbali zikiwemo za kiuchumi na kijamii.

    Aliongeza kuwa nchi yake imekuwa rafiki wa kweli na Tanzania na imekuwa mstari wa mbele kuongeza misaada yake kwa Taifa hilo na Afrika kwa Ujumla.

    Alisema China ilikua ni nchi ya kwanza kuiunga mkono Zanzibar mara baada ya Mapinduzi ya mwaka 1964 na ushirikiano huo umekuwa ukiendelea hadi hivi sasa.

    Naye Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Dkt. Juma Muhammed Salum alisema China imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Zanzibar na kuiletea maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, kilimo, utamaduni na michezo.

    Alikumbusha juu ya ujenzi wa hospitali ya Abdalla Mzee Pemba, ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Amanai na Mao tse Tung na kusaidia kuleta madaktari na vifaa tiba kwa ajili ya Hospitali kuu ya Mnazimmoja na ile ya Mkoani.

    Aidha alisema wameweza kusaidia ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar na miundo mbinu ya Barabara na huduma za mawasiliano kwa kuweka taa katika barabarani mbali mbali za Zanzibar.

    Alisema uhusiano uliopo kati ya China na Tanzanzia ni wa kipekee kwani Rais wa kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere alikuwa kiongozi pekee alieweza kukutana na Baba wa Taifa la China Marehemu Mao mjini Beijing mara nyingi zaidi kuliko kiongozi mwengine yoyote katika uhai wake.

    Aidha Mkurugenzi huyo alilieleza kuwa China imekuwa ikitoa elimu kwa vijana wa Zanzibar katika fani tofauti na imekuwa msaada mkubwa katika kuimarisha maendeleo ya kiuchumi Zanzibar.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako