• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mbinu za mapambano dhidi ya umaskini nchini China zinaweza kuigwa na kunufaisha nchi za Afrika

    (GMT+08:00) 2019-08-21 08:31:43

    NA VICTOR ONYANGO

    Afrika ni bara lililobarikiwa kuwa na maliasili nyingi, lakini kwa bahati mbaya nchi nyingi barani humo bado zimeendelea kukabiliwa na umaskini, ambao unatajwa kuwa ni sababu kuu ya matatizo mengine kama vile njaa, elimu duni na magonjwa. Changamoto hizo zinafanya kazi ya kupambana na umaskini iwe ngumu.

    Inatajwa kuwa karibu watu wawili kati ya kumi wanaishi katika lindi la umaskini barani Afrika, hii ikiwa na maana kuwa zaidi ya asilimia ishirini ya waafrika hawana uwezo wa kupata huduma za kimsingi zikiwemo za afya na elimu. Watu wenye matatizo ya kiafya wanakosa uwezo wa kufanya kazi na kupambana na umaskini, na watu wasio na elimu bora pia wanakuwa na changamoto ya kutokuwa na maarifa ya kutosha kupambana na umaskini.

    Katika baadhi ya nchi, tatizo la umaskini ni kubwa zaidi. Nchini Kenya kwa mfano, kwa mujibu wa SENSA ya mwaka 2009, asilimia 38 ya wakenya wapatao milioni 40 wanaishi chini ya mstari wa umasikini. Hii inamaanisha kuwa zaidi ya wakenya milioni 15 wanaishi kwa kutumia chini ya dola moja kwa siku.

    Hata hivyo changamoto ya umaskini haipo kwa nchi za Afrika peke yake. Ingawa China ni nchi ya pili kwa nguvu ya uchumi duniani, bado kuna watu wengine nchini China wanaoishi katika hali ya umaskini. Na serikali ya China imekuwa ikifanya juhudi za makusudi kuhakikisha kuwa inapunguza na hatimaye kutokomeza kabisa umaskini. Mwaka 2015, serikali ya China ilianzisha kampeni ya kupunguza umasikini, na kuweka lengo la kutomokeza umaskini katika miaka mitano. Ripoti ya serikali ya China iliyotolewa wakati wa mkutano wa Bunge la Umma la China wa mwaka huu, inaonesha kuwa kazi hiyo inaendelea vizuri, na mwaka huu watu milioni 13.86 waliondolewa kutoka kwenye lindi la umasikini.

    Kumekuwa na maswali kuwa ni kwanini China inaweza kupunguza idadi ya watu maskini kwa kasi kubwa namna hiyo? Ni mambo gani ambayo nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutoka kwa China ili kupunguza idadi ya watu maskini? Kumekuwa na majibu ya jumla kama vile kuwekeza zaidi kwenye sekta ya miundo mbinu, kupambana na ufisadi na kuchapa kazi kwa bidii. Hayo ni mambo ambayo China imeyafanya vizuri.

    Lakini kuna mambo yanayoendelea kwenye maeneo ambako kuna umaskini. Na mwaka jana kulikuwa na maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu katika maeneo ya vijijini, ambapo kilomita 208,000 za barabara zilijengwa au kukarabatiwa. Hili ni eneo ambalo lina changamoto kubwa katika nchi za Afrika, lakini itachukua muda mrefu zaidi kulifanyia kazi kwa kuwa linahitaji pesa.

    Kote nchini China, serikali imeongeza mipango kadhaa, ikiwa ni pamoja na maendeleo ya viwanda, na kutoa msaada wa kifedha kwa watu walioathirika na janga la umaskini.

    Kumekuwa na mifano ya moja kwa moja ambayo inaweza kufanya kazi sasa katika nchi za Afrika na haihitaji gharama kubwa. Kwa mfano, katika Mji wa Xi'an, mkoani Shanxi, kaskazini magharibi mwa China, serikali ya mji huo ilianzisha kile kilichoitwa "Maduka makubwa ya Kupunguza umaskini" mwezi Januari 2018, ili kukabiliana na changamoto ya masoko ya mazao ya kilimo kwa ajili ya wakulima kutoka maeneo yaliyoathiriwa na umasikini. Lengo la maduka hayo ni kukusanya mazao ya kilimo kutoka kwa wakulima wa vijiji ambavyo ni vigumu kufikika. Mpango huo umeimarisha viwango vya vijiji na wilaya masikini ili kuendeleza sekta ya kilimo.

    Ripoti ya kazi ya kupunguza umasikini ya mkoa wa Shanxi inasema, hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu, maduka makubwa yalitoa vitu zaidi ya 200 katika makundi 13 na mfumo wake wa usambazaji unahusisha miji 10 na wilaya ndogo, vyama vya ushirika zaidi ya 30 na kaya zaidi ya 900 katika mkoa huo. Mipango kama hiyo ni baadhi ya hatua ambazo nchi za Afrika zinaweza kujifunza ili kupambana na umaskini, kwa kuwatafutia wakulima masoko na kuwasaidia kupata pembejeo za kilimo.

    Katika Mkoa wa Hainan, uliopo kusini mwa China, kuna hifadhi moja ya wanyama pori inayojulikana kama Sanya Paddy Field National Park. Kwenye eneo la hifadhi hiyo, kuna mambo mawili yanayoendelea kwa wakati mmoja. Kwanza kuna kilimo cha mpunga chotara, ambapo wakulima wanaweza kupanda na kuvuna mpunga huo mara tatu kwa mwaka. Vile vile kuna mifano ya wanyama wajulikanao kama dinosaur, ambao pia huwavutia watoto. Wakulima wa huko wametumia mbinu ya kuchanganya shughuli za kilimo na utalii, ili kupambana na umaskani. Nchi nyingi za Afrika zinazojulikana kwa kuwa na mazingira mazuri ya kilimo na utalii, zinaweza kuiga uzoefu kama huu wa Sanya ili kuwasaidia wakulima wake kupambana na umaskini. Mfano huu unaonesha kuwa sio lazima mkulima kufanya shughuli za kilimo peke yake, wakati anaweza kufanya shughuli za kilimo na kuwa na shughuli nyingine zinazoweza kumwongezea kipato.

    Lakini katika shamba la chai la Wilaya ya Ningqiang ya Shanxi, wakazi wa karibu familia 600 wanapata 7,560 RMB ($1,100) kila mmoja kwa mwezi kwa kupitia vyama vya ushirika. Kulingana na chenye tuliambiwa wakati tulitembelea shamba hilo, wanapata 7560RMB kila mmoja kutoka kwa serikali but under the umbrella of the cooperatives.

    Lakini barani Afrika, fursa nyingi za kazi zinaundwa kinyume na hali halisi, ambapo kilimo ni sekta muhimu.

    Nchi za Afrika zinazojiunga na Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" (BRI) la China zinahitaji kushirikiana zaidi na China na kujifunza mambo ya kupambana na umaskini na kupata ufahamu zaidi juu ya jinsi ya kushughulikia upungufu wa makazi. Inaweza hata kuiga mipango hiyo kwa sababu uchumi wake unasaidiwa na sekta ya kilimo.

    Kwa kumalizia, pamoja na maliasili, bidhaa za kilimo na nguvu za utalii, serikali za nchi mbalimbali za Afrika zinaweza kugonga haya yote kwa lengo la kukomesha umaskini licha ya kukabiliana na rushwa na kutetea uwazi katika sekta zote za serikali.

    Kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, karibu nusu ya watoto wote wa Afrika eneo la Kusini mwa Sahara wanaishi katika umaskini uliokithiri.

    Ni kwa ujasiri kwamba nchi za Afrika zinahitaji kujifunza mambo fulani kutoka kwa China juu ya jinsi ya kupambana na umasikini na ufisadi ambao unakula uchumi.

    Ingawa watu wanaoishi chini ya mstari wa umasikini nchini China (yaani wanatumia chini ya dola 3 za Marekani kwa siku) wanapata maji safi, miundo mbinu nzuri, umeme na huduma nzuri ya afya pamoja na makazi bora, wako ambao bado wanaendelea kuishi katika hali ngumu. Lakini watu kama hao katika nchi za Afrika wanaishi kwenye mazingira magumu zaidi.

    Nchi za Afrika zinaweza kushirikiana zaidi na China katika sekta ya miundo mbinu. Kwa mfano Kenya inaweza kupanua ushirikiano na China kutoka kwa miundo mbinu ya sasa ambayo inajumuisha Reli ya Mombasa-Nairobi kwenda kwenye nyumba ili kurekebisha upungufu wa makazi milioni 2 kwa sasa.

    Kuanzia mwanzo wa miaka ya 1990, watu wa China wamefanya kampeni za nguvu ili kuondokana na rushwa na kuwalipa viongozi hao wa serikali ambao walitumia fedha za umma kwa ufanisi kama njia ya kuvutia wawekezaji kwa uchumi kukua.

    China imeendelea kuimarisha ugatuzi na kuzipatia nguvu zaidi mamlaka za mitaa ili ziweze kufanya maamuzi ya haraka na muhimu ili kuvutia na kuimarisha uwekezaji.

    Wavunaji wa majani ya chai katika shamba la chai

    Maonesho ya sanaa ya chai

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako