• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madaktari bingwa waliosoma China Wafanya kampeni ya  upimaji magonjwa yasiyoambukiza Kisarawe

    (GMT+08:00) 2019-08-30 17:18:23
    Na Theopista Nsanzugwanko, Dar es salaam

    WAKAZI wa Kisarawe mkoani Pwani, takribani 1,000 watanufaika na kambi ya kwanza ya kampeni ya uchunguzi na matibabu dhidi ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza, inayotolewa na madaktari bingwa wa Jumuiya ya Watanzania Waliosoma China (DCAT).

    Mwenyekiti wa DCAT, Dk. Liggyle Vumilia anasema katika siku hizo tatu, watachunguza afya watu 600 hadi 1,000 wa magonjwa ya saratani, moyo, kisukari na mengineyo.

    "Kampeni yetu ina kauli mbiu 'Jali Afya yako, Fanya Uchunguzi Mapema', tunalenga wananchi wa kawaida, tunawahamasisha wajenge tabia ya kuchunguza afya zao, itawasaidia kujua mapema kama wanakabiliwa na matatizo au la!," anasema.

    Mkuu wa Wilaya hiyo ya Kisarawe, Jokate Mwegelo anasema utoaji wa huduma bora za afya ni miongoni kwa vipaumbele vya serikali ya Rais Magufuli na msisitizo zaidi ni utoaji wa huduma za kinga.

    Akifungua kambi hiyo, katika hospitali ya wilaya ya Kisarawe waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Suleiman Jaffo Anawahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujua hali zao.

    Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Kisarawe, anamuomba Mwambata wa Ubalozi wa China anayeshughulikia masuala ya utamaduni na elimu, Gao Wei ambaye alimwakilisha Balozi wa China, kwamba China waijengee hospitali hiyo jengo la kisasa la matibabu.

    "Tunashukuru wataalamu wetu wameona katika kampeni hii Kisarawe iwe ya kwanza kisha watakwenda maeneo mengine ya nchi, Rais John Magufuli anatujengea jengo la kisasa la OPD (wagonjwa wa nje) hapa Kisarawe," alisema.

    Alisema uhusiano wa Kisarawe na China ni wa miaka mingi tangu wakati wa ujenzi wa reli ya Tazara. Alisema sasa wigo wa uhusiano huo umepanuka mpaka kwenye elimu, afya na sekta nyinginezo.

    Anawasihi wakazi wa Kisarawe kuitumia vizuri fursa hiyo ya uchunguzi. Alisema wenye wagonjwa nyumbani, wawapeleke hospitalini hapo kwa kuwa madaktari wabobezi, watakaochunguza na kugundua matatizo yao

    Kuhusu ombi hilo la Jafo, Mwambata huyo wa Ubalozi alisema amelipokea na kuridhia kwamba China ipo tayari kujenga jengo la kisasa katika hospitali hiyo.

    Anasema ushirikiano wa China na Tanzania ni wa miaka mingi na China ;na mfano China imekuwa ikitoa ufadhili kwa Watanzania kwenda kusoma elimu mbalimbali nchini humo .

    Anasema wanafurahi kuona wataalamu waliopata ufadhili wa masomo China, sasa wanasaidia nchi katika mambo mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako