• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sarafu ya dijitali ya China kusubiri

    (GMT+08:00) 2019-09-27 13:55:19

    NA VICTOR ONYANGO

    BEIJING, CHINA

    Mpango wa China wa kuzindua sarafu ya dijitali italazimika kusubiri muda mrefu zaidi kulingana na Gavana wa Benki ya Watu wa China, Yi Gang.

    Akizungumza na waandishi wa habari Jumanne mjini Beijing kabla ya maadhimisho ya miaka 70 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya watu wa China, Gavana Yi alisema kwa sasa, benki kuu haijafikia tamati kuhusu kuanzisha utumiaji wa sarafu ya dijiti nchini.

    "Kuhusu suala la sarafu ya dijitali, hadi sasa, hatujasadikishwa na utafiti wetu kwamba tunaweza kuianzisha kwa watu wetu kwa hivyo hakuna ratiba yake basi watu wataendelea kusubiri hadi siku tutakuwa tumeridhishwa na utafitu tunaofanya kwa sasa, " asema bwana Yi.

    Alifafanua kuwa benki kuu kwa kushirikiana na wizara ya fedha, wanaendelea na uchunguzi yakinifu juu ya sarafu ya dijiti ikiwa ni pamoja na tathmini ya hatari zinazotokea wakati wa utumiaji wake.

    Aliongeza kuwa "lazima tugundue ikiwa aina hii ya dijiti itatumika katika kuvuka mpaka ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na mashirika ya vyombo vya ujasusi vya pesa."

    Nchi ya China mnamo 2014 ilikuja na wazo la kupakua sarafu yake ili kupunguza gharama ya kuzunguka fedha za jadi za karatasi ili kuongeza ufuatiliaji wa mzunguko wa sarafu nchini humo.

    Gavana alihakikishia nchi hiyo kuwa Yuan iko imara akisema kuwa sera ya nchi hiyo ni ya busara na ya kawaida licha ya Yuan kushuka thamani dhidi ya dola ya Marekani.

    "Ulimwengu unakabiliwa na shinikizo la kushuka kiuchumi lakini uchumi wa China unabaki thabiti na sera za fedha zinatoa nafasi ya marekebisho zaidi," asema Gavana Yi.

    Kulingana na waziri wa fedha Liu Kun, China imepiga hatua kubwa katika mifumo yake ya kifedha kwa miongo saba iliyopita kutoka takriban dola bilioni moja mnamo 1950 hadi dola trilioni tatu mnamo 2018.

    Aliongeza kuwa nchi ya China itaendelea na kufungua mageuzi kwenye uchumi wake kwa gharama inayoendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako