• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tuna mengi ya kujifunza China, makamu wa Rais wa Tanzania asisitiza

    (GMT+08:00) 2020-01-21 14:54:05

    Na Majaliwa Christopher

    MAKAMU wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema nchi hiyo ya Afrika Mashariki ina mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa China katika juhudi zake za kuboresha maisha ya watu na kufanya Mageuzi makubwa ya kiuchumi.

    Alisema kuwa China imepiga hatua kubwa ya Maendeleo kiuchumi ambayo imeendana na kuboresha maisha ya wananchi wake -- hivyo kuwa mfano bora kwa Tanzania kujifunza.

    Makamu wa Rais alisema hayo Jumamosi jioni, Januari 18, 2020 jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe za Mwaka Mpya wa Kichina, shughuli iliyohudhuriwa na mamia ya Wachina wanaoishi Tanzania, mabalozi mbalimbali na viongozi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano, George Simbachawene, Kiongozi huyo alisema uhusiano wa China na Tanzania unazidi kuimarika na kufaidisha wananchi wa nchi hizo mbili.

    "China imekuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni. Mkakati wake wa kuondoa wananchi milioni 10 kwenye umaskini kila mwaka ni jambo la kuigwa na kutekelezwa kwa nguvu zote," alisema makamu wa Rais.

    Alisema kuwa pamoja na kuwa Tanzania na China wamekuwa na urafiki wa miaka mingi, Watanzania wana mambo ya msingi ya kujifunza kutoka kwa nchi hiyo ya pili kwa utajiri duniani ambayo pia ina idadi kubwa ya watu.

    Alisema mikakati ya China iliyojiwekea katika kupambana na umaskini uliyosaidia nchi hiyo kuondoa takribani watu milioni 700 kutoka kwenye umaskini umeifanya nchi hiyo kuwa mfano bora duniani.

    "Tuendelee kushikana mikono ili tuweze kusonga mbele pamoja huku tukiimarisha na kuweka nguvu katika mahusioano yetu ya Kidiplomasia kwa kuwa tukifanya hivi tutazidi kupata faida na pia wananchi wetu kunufaika zaidi," alisema mama Samia.

    Katika maadhimisho hayo Balozi wa China nchini Tanzania Wang Ke aliwaongoza Wachina waishio nchini katika maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.

    Michezo mbalimbali ya Kichina ilikuwa kivutio kikubwa kwenye ukumbu wa sherehe hizo.

    Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Wang alisisitiza umuhimu wa kuendelea kudumisha na kuimarisha uhusiano wa China na Tanzania kwani katika kipindi cha zaidi ya miaka 50 nchi hizo zimefadika sana na ushirikiano huo.

    Sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa kichina ni sikukuu kubwa kabisa kwa Wachina katika mwaka mzima ambayo ni kama sikukuu ya Krismasi katika nchi za Magharibi au za Afrika.

    Ingawa namna ya kusherehekea sikukuu hiyo inabadilika badilika kutokana na jinsi muda unavyokwenda, lakini nafasi muhimu ya sikukuu hiyo katika maisha ya Wachina haibadiliki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako