• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mitazamo mbalimbali kuhusu matumizi ya Mask wakati wa janga la virusi vya Corora

    (GMT+08:00) 2020-04-17 17:09:21


    Wakati dunia bado haina maoni ya pamoja kuhusu matumizi ya mask na ufanisi wake kwenye kupambana na virusi vya Corona, kumekuwa na mwelekeo unaoonyesha kuwa matumizi ya mask ni muhimu na yanaweza kumwepusha mtu kuambukiza au kuambukizwa virusi vya Corona. Wataalamu wa afya na Shirika la Afya Duniani WHO katika nchi za magharibi walikuwa wanashauri kuwa mask zinatakiwa kuvaliwa na wafanyakazi wa afya walioko kwenye mstari wa mbele wa kupambana na virusi hivyo, na wagonjwa wa virusi vya Corona ambao wanaweza kuambukiza wengine.

    Hata hivyo ushauri huo umekumbwa na maswali kutoka kwa wafuatiliaji wa maswala ya afya, hasa kutokana na ukweli kwamba nchi zenye utamaduni wa matumizi ya mask, na zilizotumia mask kwa wingi katika kupambana na virusi vya korona kuwa na viwango vidogo vya maambukizi, ikilinganishwa na nchi ambazo zilipuuza matumizi ya mask.

    Hivi karibuni waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe alitangaza hatua ya kuwalazimisha wasafiri wote nchini Kenya wavae mask, hali ambayo imeashiria mabadiliko makubwa ya sera.

    Nchini Marekani, kufuatia pendekezo la Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, matumizi ya Mask yameanza kupewa kipaumbele. Kwa sasa wale wasio na mask, wanaweza kutumia leso au Bandanaļ¼Œkatika baadhi ya nchi za Ulaya zimetungwa kanuni kali ambazo mtu anaweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini kubwa kutokana na kutovaa mask. Hata hivyo hatua hizi ambazo zilitakiwa kuchukuliwa tangu mwanzo, zinachukiwa sasa wakati hali ya maambukizi katika baadhi ya nchi imekuwa mbaya, na kwenye baadhi ya nchi za Afrika mjadala unaendelea huku idadi ya wanaoambukizwa ikiendelea kuongezeka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako