|
Hivi sasa hali ya maambukizi ya virusi vya Corona inaelekea kuwa nzuri, na kwenye ripoti ya uchunguzi iliyotolewa na Jopo la Washauri bingwa la Uingereza Deep Knowledge Group, China inashika nafasi ya tano duniani kati ya nchi zinazochukuliwa kuwa ni salama zaidi wakati wa janga hili. Katika mapambano hayo dhidi ya ugonjwa, China imeonesha uwezo na uwajibikaji na udhati, ambao si kama tu ni mali kwa wananchi wa China, bali pia ni mali ya pamoja kwa watu wote duniani na jumuiya ya binadamu duniani.
Tangu maambukizi ya virusi vya Corona yalipotokea nchini China, hatua mbalimbali za kuzuia na kudhibiti za China zimeonesha kasi na ufanisi wa China.
Maelfu ya wafanyakazi wa matibabu walikwenda mjini Wuhan mkoa wa Hubei kutoa msaada, hospitali mbalimbali zilijengwa ndani ya muda mfupi, na misaada mingi ya vitu vya matibabu ilisafirishwa kwenda kwenye sehemu zilizoathiriwa vibaya zaidi na janga hili. Takwimu kutoka Shirika la Afya Duniani WHO zimeonesha kuwa, hali ya maambukizi ya virusi vya Corona ilitulia baada ya kufika kilele kuanzia tarehe 23 Januari hadi tarehe 2 Februari, na kuendelea kushuka.
Uwezo wa China unategemea hali yake ya mfumo wa kisiasa. Tarehe 23 Februari, rais Xi Jinping wa China alieleza kwenye Mkutano wa mipango ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona na kazi ya maendeleo ya kiuchumi na ya kijamii kuwa, mafanikio ya China katika kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo yameonesha sifa dhahiri ya uongozi wa chama cha kikomunisti cha China, na mfumo wa Ujamaa wenye umaalum wa China.
Matukio ya dharura ya afya ya umma ni changamoto ya pamoja inayowakabili binadamu wote, na inahitaji ushirikiano wa nchi zote duniani. Ili kukabiliana na janga hili kubwa, China inafanya juhudi kubwa, na kuchukua hatua mwafaka ambazo zimetoa mfano mzuri wa kuigwa kwa kazi ya kuzuia ugonjwa huo duniani. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, wananchi wa China wamepata hasara kubwa katika kuzuia maambukizi ya virusi, huo ni mchango muhimu kwa binadamu wote. Mshauri mwandamizi wa katibu mkuu wa WHO Bw. Bruce Elward, pia ameeleza kuwa China imetoa mchango mkubwa kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona, na kuokoa muda muhimu kwa nchi na sehemu nyingine duniani katika kuzuia ugonjwa huo.
China inapopambana kwa pande zote na ugonjwa huo, inafanya ushirikiano na kubadilishana habari zinazohusika na WHO, kufanya utafiti juu ya vitendanishi vya upimaji, kubadilishana uzoefu kuhusu kuzuia ugonjwa na nchi zinazohusika, na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kuhusu dawa na chanjo, na kutoa misaada kwa nchi na sehemu zinazoathiriwa vibaya na janga hili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |