• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maelewano na ushirikiano wa wananchi wa China vyaweka msingi thabiti kwa kushinda mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-05 09:10:35


    Katika mapambano magumu dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona, ili kuzuia kwa kiasi kikubwa ugonjwa huo, serikali ya China imekuwa ikitoa wito kwa wananchi kujilinda, na kupunguza safari zisizo za lazima. Ingawa janga hili lilitokea wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China, ambapo ni wakati muhimu kwa familia za wachina kujumuika na kusherehekea kwa pamoja, lakini ni wajibu kwa wananchi kufuata maagizo ya kujikinga, na kufahamu umuhimu wa "kukaa nyumbani vilevile ni kutoa mchango". Wananchi wa China wanafahamu vizuri kuwa kushinda mapambano dhidi ya ugonjwa huo kunategemea nidhamu na kufuata maagizo.

    Uchunguzi kutoka Shirika la uchunguzi wa maoni la Uholanzi Glocalities, umeonesha kuwa mlipuko wa maambukizi ya virusi vya Corona unawafanya wachina watilie maanani zaidi kanuni na nidhamu, na kuwa na hamu kubwa zaidi kwa utaratibu na kufahamu vizuri kutoa shukrani kwa michango ya watu wengine.

    Matokeo yenye ufanisi yaliyopatikana na China katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo yanategemea utaratibu wa kuzuia na kudhibiti magonjwa ulioanzishwa na serikali, jambo lingine muhimu ni kiwango cha juu cha maelewano na utii wa wananchi wa maagizo. Katika miezi miwili iliyopita, wananchi wengi wa China walichagua kukaa nyumbani ili kujikinga dhidi ya virusi, wakati mashirika mengi yanatoa misaada ya uzalishaji wa vifaa vya matibabu, usambazaji wa bidhaa kwa njia ya kutumia kwa pamoja wafanyakazi au sehemu za uzalishaji, na watumishi wa ngazi ya mitaa walibeba majukumu ya wasimamizi wa afya. Kila mtu wa kawaida anafuata maagizo na nidhamu kwa makini, hali ambayo inatoa mchango katika kazi ya kuzuia na kudhibiti ugonjwa kote nchini China. Maelewano na ushirikiano wa wananchi wote wa China viliweka msingi imara wa ushindi kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako