Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini Marekani imezidi laki 8.6, idadi ya vifo imezidi elfu 49.
Hali ya maambukizi ya virusi vya Corona imeathiri vibaya uchumi duniani. Takwimu kutoka Wizara ya kazi ya Marekani zinaonyesha kuwa, kadiri hasara zinazotokana na maambukizi ya virusi vya Corona zinavyoongezeka, na wamarekani wengi wanazidi kupunguzwa kazini. Wiki iliyopita wamarekani wengine milioni 5.2 wamepunguzwa kazini na kuomba msaada wa fedha kutoka serikalini. Tokea tarehe 21 Mwezi Machi, watu zaidi ya milioni 22 nchini Marekani waliomba msaada wa fedha kutokana na kupunguzwa kazini, kiasi ambacho ni asilimia 13.5 ya idadi ya jumla ya wafanyakazi wa nchi hiyo.
Gazeti la Sera za Diplomasia limeeleza kuwa, kadiri muda wa kuchukua hatua za kuweka karantini unavyoongezeka, ndivyo athari kwenye uchumi wa Marekani zinavyozidi kuongezeka, na kasi ya kufufuka kwa uchumi inazidi kupungua. Kutokana na hali hii, rais Donald Trump wa Marekani ameharakisha mchakato wa kufufua uchumi. Gazeti la Time limeripoti kuwa, Tarehe 16 Aprili rais Trump alitangaza mwongozo wa kurejesha uchumi, na kukabidhi madaraka ya kuondoa karantini ya kukaa nyumbani kwa magavana wa majimbo mbalimbali. Hata hivyo wachumi wameeleza kuwa, bado muda unahitajika kwa wananchi wa Marekani kuweza kuishi kwa utulivu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |