Hivi karibuni, hali ya kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona nchini China inaonesha mwelekeo mzuri, huku makampuni mengi yakiwa yanarejesha shughuli zao hatua kwa hatua. Lakini hii haimaanishi kuwa tahadhari juu ya maambukizi ya ugonjwa huo imeondolewa, au mapambano dhidi ya ugonjwa yamemalizika.
Tarehe 9 Aprili, mtu mmoja alithibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona kwenye mji wa Harbin, mkoani Hei Longjiang, hali ambayo imevunja rekodi ya mkoa huo kwa kutokuwa na mtu wa kuambukizwa virusi hivyo kwa siku 29 mfululizo. Kwa mujibu wa Kamati ya Afya ya Mkoa wa Heilongjiang, hadi sasa idadi ya watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi kutokana na yeye imefikia 70.
Ofisa wa kamati hiyo Bw. Xie Yunlong ameeleza kuwa, sababu ya tukio hilo ni kuwa, kutokana na kupunguzwa kwa kiwango cha kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo, baadhi ya watu wamelegeza tahadhari, huku hali ya watu kujumuika ikiongezeka. Utafiti umeonesha kuwa, matukio mawili ya maambukizi ya virusi mkoani Heilongjiang yanatokana na kujumuika kwa watu.
Akizungumzia sababu nne za watu kuambukizwa hospitali, Bw. Xi amesema baadhi ya wafanyakazi wa matibabu hawakuwa makini kwenye masuala ya kinga, kutochukua hatua ya kusimamia kwa makini watu wanaoingia wodini, kutotekeleza kwa makini utaratibu wa kuzuia magonjwa ya kuambukiza hospitalini, na baadhi ya wakuu wa hospitali kutoweka mkazo katika kazi ya kuzuia maambukizi ya virusi. Kwa hiyo alilazimika kutoa wito kwa wananchi kutojumuika na kufuata kwa makini kanuni zinazohusika za kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi, pia amezitaka hospitali ziimarishe utekelezaji wa utaratibu makini wa usimamizi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |