"Somo la mafunzo kazi" halitakiwa kubaki kwenye nadharia tu. Mbali na kufundishwa darasani, ni bora zaidi kuwatoa fursa kupata uzoefu halisi.
Hivi karibuni, shule moja ya mkoa wa Heilongjiang ilianzisha shughuli ya kusafisha theluji. Msichana mwenye umri wa miaka 13 alisafisha kwa karibu saa tatu bila glovu, na kuumia vidole vyake kutokana na baridi kali, na kuwa hatarini ya kukatwa. Baada ya tukio hilo, baadhi ya vyombo vya habari vya mtandao wa Internet vimezusha mjadala wa " Je, inafaa kuwafanya wanafunzi wafanye kazi kwa ajili ya shule bila malipo?" Na baadhi ya watu wanaona hiyo sio kazi ya wanafunzi.
Bila shaka wanafunzi wanaumia kutokana na muda mrefu wa kufanya usafi kuondoa theluji, shule ni lazima ibebe majukumu ya usimamizi wa usalama. Lakini kinachotia shaka ni kwamba kuwafanya wanafunzi wafanye kazi za shule bila malipo kunawaweka wanafunzi na shule kwenye pande mbili zinazovutana.
Kama wanafunzi wanafanya kazi shuleni kwa njia mwafaka haipaswi kuchukuliwa kuwa shule "inahitaji" wanafunzi kufanya kazi, bali ni sehemu ya elimu ya shule. Kwani mafunzo kama hayo ni kipimo muhimu cha uwezo wa wanafunzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |