Katika Baraza la uwezo wa uongozi wa wakuu wa shule lililofanyika tarehe 6 Januari, mwanzilishi wa kundi la Alibaba aliwahi kuwa mwalimu wa kiingereza na biashara ya kimataifa katika Chuo cha viwanda vya kielektroniki cha mji wa Hangzhou, alisema ingawa ameondoka katika sekta ya elimu kwa miaka mingi, lakini amegundua matatizo yanayokabili sekta hii. Amesema baada ya kufanyika kwa uchunguzi, chanzo kuu kwa walimu wengi wa vijijini kuhama shule ni kutoridhika na wakuu wa shule. Kiwango na uwezo wa usimamizi cha wakuu wa shule kinaamua mwelekeo wa maendeleo ya shule, walimu na wanafunzi. Kama wakuu hawana mtazamao wa kuangalia siku za baadaye, walimu hawataona mustakabali wao.
Bw. Ma Yun amesema wakuu wazuri wa shule wanategemea mitizamo ya kuangalia mustakabaliwao, uwajibikaji wao wa majukumu, utaratibu na hatua halisi za utekelezaji. Katika vijiji vilivyoko mbali, wakuu wa shule ni kama waziri wa elimu wa huko, si kama tu wanaathiri shule zao, bali pia kiwango cha elimu ya huko, hata kiwango cha uchumi, na utamaduni cha huko. China ina wakuu laki 2 wa vijijini, kama wakuu hao watafundishwa vizuri, watoto milioni 60 watakuwa na mustakabali mzuri.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |