Katika miaka kumi iliyopita, idadi ya watu wasiofunga ndoa nchini China imefikia milioni 200, huku uchumi wa aina mpya wa kuwahudumia watu kama hao ukiibuka.
Hivi karibuni Mgahawa mmoja wa Hotpot kwa mtu kula peke yake umekuwa unakaribishwa sana mjini Chengdu.
Ndani ya mgahawa huo, meza ya chakula inatengwa kumfaa mtu mmoja, lakini inaweza kubadilishwa kama watu wakitaka kula kwa pamoja. Hakuna wahudumu wamnaotembea ndani ya mgahawa huo, na huduma zote zinatolewa nyuma ya pazia kati ya meza ya chakula na jiko.
Msichana Wang Zhenzhen aliyezaliwa baada ya mwaka 1980 ni mmiliki wa mgahawa huo, alianzisha biashara hiyo mwaka 2018 wakati alipotalii Chengdu peke yake. Wakati ule, aliwahi kwenda kwenye mgahawa uliojulikana sana wa Hot Pot, palikuwa na watu wengi, na alikuwa mtu pekee aliyekuwa anakula peke yake, hali ambayo ilimfanya ajisikie vibaya. Alifikiri kuwa kama ataanzisha mgahawa kwa mtu kula peke yake, utavutia vijana wengi.
Wang Zhenzhen anasema hivi sasa vijana wanakabiliwa na mashinikizo mbalimbali, na pia wengi wana elimu ya juu, wamezoea kuishi kwa kujitegemea, mgahawa huo unatoa nafasi kwa watu kama hao kujiburudisha kwa muda wa kula peke yao kwa utulivu, bila ya kusumbuliwa na watu wengine.
Kijana Feng Xuegang anatembelea mgahawa huo mara tatu hadi nne kila mwezi, na kila mara anapenda kula hotpot huku akitazama video kwenye simu yake ya mkononi. Anasema anafurahia wazo la mgahawa huo, kwani si lazima watu wanapaswa kula pamoja mgahawani, na mtu anaweza kuburudika kwa kula chakula peke yake bila upweke, hali hii inalingana sana na mahitaji ya vijana kwa hivi sasa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |