• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mahali maalumu pa kuegesha gari kwa wanawake

    (GMT+08:00) 2020-06-03 09:44:33






    Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na maeneo maalum ya wanawake kuegesha magari nchini China. Jambo linalozingatiwa ni kuwa sehemu na wazi zaidi ili kuleta urahisi wa kuegesha gari. Lakini wakati baadhi ya wanawake wanafurahia hatua hii, wengine wanailaani kama ni aina ya ubaguzi wa kijinsia.

    Bibi Zhao ambaye ameendesha gari kwa miaka miwili, amesema yeye si hodari wa kuendesha gari, hususan wakati wa kurudisha nyuma gari, kwa hiyo kwake ni jambo zuri na la kufurahisha.

    Wanamtandao wengi pia wametoa maoni yao, baadhi wamesema maeneo hayo yanaandaliwa kutokana na kuwa wanawake wanachukuliwa kuwa na uwezo mbaya wa kuendesha gari, na ni aina ya ubaguzi wa kijinsia. Wengine wanaona ni jambo la kawaida kwa maeneo maalum ya madereva wanawake kuwa karibu na mlango wa kutoka na kuwapa urahisi mkubwa, hatua ambayo imeonesha vya kutosha moyo wa dhati, na isitafsiriwe kuwa ni uwezo mdogo wa wanawake kuendesha na kuegesha magari au ubaguzi wa kijinsia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako