Bwana harusi kutoa mahari kwa bibi harusi kabla ya kufunga ndoa, ni mila inayoenziwa kutoka enzi za kale. Ingawa tumeingia katika zama mpya, lakini mila hii bado inaendelea kudumishwa. Lakini hivi sasa baadhi ya wazazi wanachukua vigezo viwili juu ya suala hilo, wakiona kuwa mahari anayoidai bibi harusi ni kubwa wakati mtoto wao akifunga ndoa, lakini wanapoozesha nao hudai mahari kubwa.
Bibi Li ana watoto wawili mmoja wa kiume na mwingine wa kike, alipoongea na jirani wyke alilalamika kwamba, mtoto wake wa kiume ametimiza miaka 35 na amepata mchumba, lakini alidaiwa mahari ya yuan laki 1.5, dai hili lilimkasirisha sana Bibi Li, alisema, "sasa imekuwa zama mpya, mbona wanadai mahari? Hiki ni kitendo cha kumuuza binti, si ndiyo?" Lakini na yeye alipoulizwa kama atadai mahari wakati binti yake atakapoolewa, alijibu "Kwa nini nisidai mahari? Nimemlea kwa zaidi ya miaka 20, ni lazima haitapungua yuan laki 2.5." . Ni akili kama hizo ndio zinafanya mtoto wa Bibi Li mwenye umri wa miaka 35 awe bado hajaoa. Kuna watu wengi wenye mtazamo wa Bibi Li, wanaoona mabinti zao ni wazuri zaidi na wana thamani kuliko wa wengine. Tabia ya kudai mahari kimsingi ni kuleta ukaribu kwa watakaofunga ndoa, na familia nyingi zinakubali desturi hiyo ikiwa katika viwango mwafaka. Tabia ya kushindana wakati wa kudai mahari au kuwa na vigezo viwili juu ya suala hilo, inaonekana kuyumbisha uhusiano wa kifamilia.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |