• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfanyakazi wa benki aliandika kwa makosa yuan 300 kuwa 49,000 kwenye akaunti ya mteja na kukataliwa kurejeshwa

    (GMT+08:00) 2020-06-26 15:34:40


    Hivi karibuni mwanaume mmoja alikwenda benki kuweka akiba ya fedha, lakini mfanyakazi wa benki aliandika yuan 300 kuwa 49,000 kwenye akaunti yake kwa makosa. Mfanyakazi huyo aligundua kosa lake wakati benki hii ilipomaliza kazi jioni, na kuwasiliana na mteja kumdai arejeshe yuan 48,700.

    Lakini mwanamume huyo alikataa kumrejesha kwa kisingizio kwamba ni rafiki yake aliyemtunia fedha hizo, na alizitumia fedha hizo kulipa mikopo yake kwenye kadi za mikopo.

    Benki hii ikatoa mashitaka mahakamani. Mwanamume huyo aligundua kosa lake baada ya shauru mahakama, na kukubali kurejesha fedha kidogo kidogo.

    Watumiaji wa mtandao wa Internet wamekuwa na maoni tofauti kuhusiana na hili. Baadhi yao wanaona kanuni ya benki ni "kutowajibika baada ya wateja kuondoka kutoka kaunta, na mfanyakazi wa benki aligundua kosa lake baada ya mteja kuondoka, bila shaka mteja hana haja ya kuwajibika. Wengine wanaona bila ya kujali kama ni mfanyakazi wa benki aliyefanya kosa au la, mwanamume huyo alichukua pesa asiyestahiki, ni tabia mwafaka kwake kuzirejesha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako