• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwongo na Njama: jinsi Marekani inavyodanganya watu wake na jamii ya kimataifa kuhusu virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-05-21 20:47:48


    Katika hospitali ya Elmhurst jimbo la New York nchini Marekani, mchana na usiku, madaktari na manesi wanajitolea kuokoa maisha ya wagonjwa wa COVID-19, ambao hofu za kuhuzunisha zinaonekana machoni mwao, lakini bado wanashindwa kumsaidia kila mmoja. Nje ya hospitali, friji kubwa zimepangwa kwa foleni katika uwanja wa kuegesha magari ili kuhifadhi miili ya marehemu kwa sababu vyumba vya kuhifadhi maiti hospitalini hapo vimejaa.

    Wakati idadi ya watu waliofariki kwa COVID-19 ilipozidi elfu 10 katika jimbo la New York, gavana Andrew Cuomo alisema janga hilo linatisha na kuleta uchungu na hasara kubwa. Sasa miezi miwili imepita na idadi hiyo imeongezeka kwa mara karibu 3. Na Marekani inaongoza dunia katika kipindi hicho kwa kuwa na watu zaidi ya milioni 1.48 walioambukizwa virusi vya Corona, huku zaidi ya watu karibu elfu 90 wakiaga dunia.

    Kama waandamanaji wa Marekani wanavyouliza, ni nini kimetokea na kuifanya nchi yao ishindwe kabisa kudhibiti virusi vya Corona? Jibu ni kwamba, serikali ya nchi hiyo imetumia nguvu na muda wake mwingi kusambaza nadharia za njama. Watu husema, uwongo ukiurudia mara 1,000 unakuwa ukweli. Basi hebu tujaribu mara 1,001.

    Kauli ya kuitaka China kuomba radhi na kulipa fidia kutokana na janga la COVID-19 duniani

    Tangu virusi vya Corona vilipuke nchini Marekani mwezi Machi, rais Donald Trump na mtiifu wake mkuu, waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo wamekuwa wakijitahidi kuikosoa China kwa kitu, wakisema China haikutoa ipasavyo taarifa zinazohusiana na COVID-19.

    Pia ni kuanzia mwezi huo huo, televisheni ya Fox News ya Marekani inayochukuliwa kuwa ni msemaji wa Chama cha Republican imejitahidi kuishambulia China ama kwa kupitia watangazaji wake au kwa kuwaalika wageni. Kwa mfano, tarehe 7, Aprili, aliyekuwa mshauri mkuu wa mkakati wa rais Donald Trump wa Marekani Steve Bannon alihojiwa na televisheni hiyo akisema, "imethibitishwa na China pia imeonesha kuwa COVID-19 ni mauaji ya kupangwa. Tarehe 18, Aprili, mtangazaji wa Fox News Jeanine Ferris alisema, "China inafahamu vya kutosha chanzo cha virusi vya Corona, lakini inatoa taarifa zisizo za kweli" Tarehe 21, Aprili, mwanasheria mkuu wa jimbo la Missouri Eric Schmitt aliiambia Foxnews kuwa atafungua mashtaka dhidi ya China.......

    Tarehe 23, Januari, serikali ya China ilifunga mji wa Wuhan. Kuanzia hapo, baadhi ya nchi zilichukua hatua za kutosha na kufanikiwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona ndani ya nchi, lakini Marekani imekuwa nchi iliyoshindwa kabisa kudhibiti virusi hivyo duniani.

    Akijibu shutuma zilizotolewa na wanasiasa hao wa Marekani dhidi ya uwazi wa China katika kukabiliana na ugonjwa huo, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying aliuliza maswali matatu: kama China ingeficha kwa makusudi hali halisi ya maambukizi ya virusi hivyo, kwa nini Marekani ilikuwa nchi ya kwanza kuwarejesha nyumbani wafanyakazi wake katika ubalozi mdogo wa Marekani mjini Wuhan? Kwa nini Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa cha Marekani CDC hakikutoa takwimu kuhusu maambukizi ya ugonjwa huo nchini humo na hata kufuta takwimu zilizoonesha kuwa kulikuwa na maambukizi 171 katika jimbo la Florida mapema mwezi Januari katika tovuti yao? Na vipi kuhusu kumbukumbu yenye kurasa 57 iliyofichuliwa na vyombo vya habari inayoonesha kuwa timu za kampeni za Chama cha Republican zimeshauriwa kuishambulia China wakati zinaposhughulikia shutuma kuhusu virusi vya Corona ndani ya nchi hiyo?

    Jaribio la kuvihusisha virusi vya Corona na maabara Wuhan ili kuanzisha vita dhidi ya China kama ilivyofanya dhidi ya Iraq

    Tarehe 30, Aprili, rais Donald Trump alisema kwenye Ikulu ya Marekani kuwa amesoma ushahidi unaoaminika sana unaoonesha kuwa virusi vya Corona vilitoka kwenye maabara mjini Wuhan, lakini alipoulizwa ni ushahidi gani, alikataa kusema.

    Tarehe 3, Mei, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alikuwa na mahojiano yafuatayo na mtangazaji na Shirika la Utangazaji la Marekani ABC kuhusu kama virusi vya Corona vilitengenezwa na binadamu:

    Pompeo: Nina ushahidi mwingi wa kuthibitisha kuwa virusi vya Corona vilitoka kwenye maabara mjini Wuhan

    Mtangazaji: Unaamini virusi hivyo vilitengenezwa na binadamu au kupangwa upya kwa jeni? (genetically modified)?

    Pompeo: Hadi sasa wataalam bora wanaona vilitengenezwa na binadamu, na sina sababu ya kukataa maoni yao.

    Mtangazaji: Lakini kwa mujibu wa ofisi ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa DNI Marekani, wadau wa sekta ya sayansi wanakubaliana kuwa virusi vya Corona havikutengenezwa na binadamu wala kupangwa upya kwa jeni.

    Pompeo: Ndio. Nakubaliana na kauli hiyo. Nimeona uchambuzi wao, sina sababu ya kutia mashaka juu ya usahihi wake.

    Mtangazaji: Basi unatakiwa kuweka bayana, huamini virusi vya Corona vilitengenzwa na binadamu au kupangwa upya kwa jeni?

    Pompeo: nimeona taarifa iliyotolewa na idara ya ujasusi, sina sababu ya kuona wao wamefanya kosa.

    Ni wazi kuwa kauli za Pompeo zimekinzana sana, mwanzoni alisema ana uhakika asilimia 100 kuwa virusi vya Corona vilitoka kwenye maabara mjini Wuhan, lakini mwisho alijichanganya na kusema anawaamini wapelelezi kuwa virusi vya Corona havikutengenezwa na binadamu.

    Tarehe 5, Mei, mkurugenzi mteule wa NDI Marekani John Ratcliffe na Mwenyekiti wa Wanadhimu Wakuu wa majeshi ya Marekani Mark Milley kwenye shughuli tofauti walisema kwa mujibu wa ushahidi wa sasa, virusi vya Corona havikutengenezwa na binadamu.

    Akizungumzia kauli hizo siku hiyohiyo, mtangazaji wa televisheni ya CNN Fareed Zakaria amesema kitu inachofanya Marekani dhidi ya China kinamkumbusha jinsi Marekani ilivyoanzisha vita dhidi ya Iraq. Rais wa Marekani na waziri wake wa mambo ya nje wanawashinikiza na hata kuwalazimisha wadau wa sekta ya ujasusi kutoa hitimisho kuwa ni China iliyosambaza virusi vya Corona. Lakini ni wazi kuwa wadau wa sekta hiyo hawako tayari kutoa hitimisho hilo ama hawataweza kupata hitimisho hilo, kwani hawana ushahidi na wameweza kufanya makosa katika kutafuta jibu.

    Mashaka yanayotiliwa juu ya Marekani kuhusu virusi vya Corona

    Tarehe 30 April, Meya wa Belleville Michael Melham alisema kwa vyombo vya habari kuwa alihisi alipata COVID-19 mwezi Novemba mwaka jana, ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya mgonjwa wa kwanza kugunduliwa nchini China, na sampuli za damu yake zimeonesha kuwa ana kinga ya mwili dhidi ya virusi vya Corona.

    Mwezi Julai, mwaka jana, taasisi ya utafiti ya kijeshi ya magonjwa ya kuambukizwa huko Fort Detrick ilifungwa kisirisiri kutokana na wasiwasi wa kiusalama. Baada ya mlipuko wa virusi vya Corona kuanza mwezi Machi mwaka huu, watu wengi nchini Marekani wameitaka serikali ieleze sababu halisi ya kufungwa kwa taasisi hiyo na pia kuchunguza ipasavyo uhusiano kati ya mafua yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya elfu 10 mwaka jana na COVID-19.

    Kuhusu chanjo dhidi ya virusi vya Corona, Rais Donald Trump wa Marekani siku zote ametetea kuwa Marekani itakuwa nchi ya kwanza duniani kutengeneza chanjo hiyo. Tarehe 15, mwezi huu, aliwaambia waandishi wa habari kuwa nchi yake ilianza kufanya utafiti juu ya chanjo dhidi ya virusi vya Corona tarehe 11, Januari. Hii inamaanisha kuwa Marekani ilianza kazi hiyo saa chache tu baada ya mpangilio wa jeni za virusi kutumwa kwenye mtandao wa internet, na miezi miwili kabla ya nchi hiyo kukumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo. Watu wengi wanajiuliza virusi ambavyo watafiti wa Marekani walitumia kutafuta chanjo vilitokea wapi? Labda jibu litaweza kupatikana baada ya Shirika la Afya Duniani WHO au jopo huru la wataalama la kimataifa kwenda Marekani kuchunguza chanzo cha virusi na jinsi inavyokabiliana na virusi hivyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako