• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  •  Wajumbe wa Bunge la Umma la China NPC watoa mapendekezo mbalimbali  yanayofuatiliwa na watu

    (GMT+08:00) 2020-05-26 16:04:40

    1. Mji wa Wuhan, China ulifungwa tarehe 23, Januari ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona ndani na nje ya China. Mjumbe Chen Jingyu ambaye ni mtaalam wa magonjwa ya mapafu kutoka mkoa wa Jiangsu alienda mjini humo kuungana na wenzake kupambana na ugonjwa wa virusi vya Corona. Safari hii ametoa pendekezo la kufanya siku hiyo kuwa siku ya afya ya umma ya taifa ili watu wa kawaida wakumbuke na kuunga mkono shughuli za afya ya umma za China. Amesema tarehe 23, Januari ilikuwa siku muhimu kwa China kuweza kufanikiwa kudhibiti virusi hivyo kutokana na kuamua kufunga mji huo.

    2. Kutokana na uamuzi uliopitishwa na Kamati ya kudumu ya Bunge la umma la China, muswada wa mwongozo wa sheria za kiraia (Civil Code) utakaowasilishwa kujadiliwa kwenye mkutano wa tatu wa awamu ya 13 ya Bunge la umma la China utaongeza "kipindi cha kutulizana baada ya kutoa ombi la talaka".

    Kwa mujibu wa kifungu hicho, ndani ya siku 30 tangu idara ya uandikishaji wa ndoa kupokea ombi la talaka, upande usiotaka kutaliki unaweza kuondoa ombi la talaka. Na pande zote mbili zinatakiwa kwenda kwenye idara ya uandikishaji wa ndoa kupokea cheti cha talaka ndani ya siku 30 zinazofuata, la sivyo inamaanisha kuwa ombi la takala limefutwa.

    Hata hivyo, mjumbe wa bunge la umma la China Jiang Shengnan ametoa pendekezo la kufuta kifungu hicho, kwani anaona kuwa lengo la kifungu hicho ni kuwazuia watu wanaotoa ombi la talaka bila kufikiri kwa makini, ili kulinda utulivu wa familia. Lakini kwa watu wengi zaidi, kifungu hicho kinaongeza muda wa uchungu unaoletwa na ndoa isiyo na furaha, na kinaweza kuzusha migongano mikubwa na hivyo kuleta athari mbaya zaidi.

    3. Mjumbe Liu Faying ambaye ni naibu mkuu shule ya msingi ya wilaya inayojiendesha ya kabila la Wa- Tu mkoani Hubei, ambayo iliondokana na umaskini mwezi Aprili tu amesema wanafunzi wa vyuo vya ualimu ambao ada zote za shule zilifutwa wanalazimika kuwa walimu, la sivyo nafasi zao za uaminifu zitakuwa mbaya. Amesema kufanya hivyo kunalenga kuinua kiwango cha elimu vijijini haswa sehemu za milimani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako