• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kuna mustakabali mzuri wa ushirikiano wa biashara kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2020-06-04 16:57:57


     


    Hivi sasa hali ya maambukizi ya virusi vya Corona imedhibitiwa kwa ufanisi nchini China, hatua ya kurejeshwa kwa uzalishaji mali imeharakishwa kote nchini, usafiri nje na matumizi ya wananchi vinarejeshwa hatua kwa hatua, maisha ya kijamii yanarejea katika hali ya kawaida, na dalili ya kufufuka kwa uchumi wa China imezidi kuwa wazi.

    Ripoti ya uchunguzi wa mazingira ya biashara ya China iliyotolewa mwaka 2020 na Shirikisho la wafanyabiashara wa Marekani nchini China inaonyesha kuwa, kutokana na mtizamo wa muda mrefu, China itaendelea kuwa soko muhimu kwa mashirika mengi ya Marekani nchini China. Gazeti la habari za uchumi wa Japan limeeleza kuwa, mashirika mengi ya Japan yanabaki nchini China, kwa sababu China imekuwa soko muhimu la bidhaa zao.

    Katika Mikutano Miwili iliyofanyika mwaka huu, ripoti ya kazi ya serikali ya China imesisitiza kwa mara nyingine kuwa, kutokana na mabadiliko ya mazingira ya nje, China itaendelea kupanua ufunguaji mlango, kutuliza mnyororo wa utoaji wa bidhaa, ili kuhimiza mageuzi na maendeleo kwa njia ya kufungua mlango. Aliyekuwa waziri wa biashara wa Uingereza Bw. Jim O'Neill, alisema China ikiwa nchi kubwa ya pili kwa uchumi duniani, ufufukaji wa uchumi wake una umuhimu mkubwa kwa kurejea kwa hali ya kawaida kwa uchumi wa dunia. Gazeti la Tanzania Mwananchi limetoa makala ikisema, nchi za Afrika zinatakiwa kufurahia ufufukaji wa uchumi wa China. Uchambuzi unaona kuwa, ufufukaji wa uchumi wa China utasaidia kuleta autulivu wa mnyonyoro ya viwanda duniani na utoaji wa bidhaa, hali ambayo itanufaisha nchi za Afrika zinazokumbwa na changamoto za afya na uchumi.

    Kutokana na janga la virusi vya Corona, nchi za Afrika zilizotegemea uuzaji wa madini ziliathiriwa vibaya. China ikiwa nchi yenye matumizi makubwa zaidi ya metali za viwanda, katika mchakato wa kufufuka kwa uchumi wake, uwekezaji wa miundo mbinu utachangia maendeleo ya sekta ya madini barani Afrika.

    Wakati maambukizi ya virusi vya Corona yalipoenea kwa kasi nchini China, shughuli za utalii na usafiri wa anga katika za nchi za Afrika ziliathiriwa vibaya, gharama za utengenezaji wa bidhaa zilipanda, na bidhaa za kielektroniki na biashara ya bidhaa ndogondogo zilikuwa haba. Kwa hiyo ufufukaji wa uchumi wa China utapunguza matatizo hayo yanayozikabili nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako