Tarehe 10 Mei ilikuwa Siku ya Mama, ambayo inatakiwa kuwa siku kwa watoto kutoa shukurani kwa kina mama. Lakini siku kadhaa zilizopita lilitokea jambo moja la kustaajabisha ambapo mwanamume mmoja Bw. Ma wa Mji wa Jingbian mkoani Shaanxi, alijaribu kumzika mama yake akiwa hai.
Ripoti inasema tarehe 5 Mei mwanaume huyo alijaribu kumzika mama yake mwenye umri wa miaka 79 akiwa hai, kwa bahati nzuri binti mke wa mtoto wake huyo aliwaarifu polisi kwa wakati na kufanikiwa kumwokoa mama huyo na kumfikisha hospitali. Hivi sasa hali ya mama huyo inaendelea vizuri, na mtoto wake anashikiliwa na polisi mwa mujibu wa sheria.
Wanakijiji wenzake walieleza kuwa mama huyo amepooeza miguu na analala kitandani tu, mara zote amekuwa ni wa kusaidiwa hata anapokwenda msalani. Kwa bahati mabaya kama Bw. Ma na mkewe wanatoka nje, bibi huyo hujisaidia kitandani, na hali hii ilimkasirisha sana Bw, Ma, na siku ile hasira yake ililipuka kama bomu na kuamua kumzika mama yake akiwa hai.
Baada ya tukio hilo kutokea, watu wengi walimlaumu vikali Bw. Ma kutokana na ukatili wake ambao umekiuka vibaya maadili na sheria. Wengine wanaona hali hii inatokana na suala la matunzo ya uzeeni linaloikabili China. Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2019, idadi ya watu wenye umri wa miaka zaidi ya 65 nchini China imefikia milioni 176, kiasi ambacho kimechukua asilimia 18.1 ya idadi ya jumla ya watu nchini China, na inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2024, kiwango hicho kitafikia asilimia 14. Serikali pia inatakiwa kuchukua hatua kushughulikia vizuri suala hili.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |