• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiini cha uhuru wa wanawake ni nini?

    (GMT+08:00) 2020-06-16 13:02:55



    Katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na mjadala hapa China kuhusu jina la ukoo analotakiwa kupewa mtoto, na kuletwa swali kama kuna ulazima wa kutumia jina la ukoo la baba. Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Internet wanaona kuwa wanawake wanaotetea moyo wa uhuru hawapaswi kufuata desturi ya kumfanya mtoto atumie jina la ukoo wa baba yake, huku wengine wakiona kitendo kama hicho hakihusiani na moyo wa uhuru wa wanawake.

    Tarehe 10 Mei, Papi Jiang ambaye anajulikana kupitia mtandao wa Internet, aliyejifungua hivi karibuni alitoa makala na picha za mtoto wake kwenye mtandao wa kijamii Weibo. Lakini alikosolewa na watumiaji wa mtandao kutokana na mtoto wake kupewa jina la ukoo la upande wa baba, na sura yake akiwa mwanamke anayetetea moyo wa uhuru imevunjika. Baadhi ya watu wanaona kumfanya mtoto apewe jina la ukoo wa mume wake ni kitendo cha kutii madaraka ya wanaume.

    Lakini tukifikiria kwa makini suala hili kutokana na mtizamo wa usawa wa kijinsia, kweli ni haki yenye usawa kwa baba na mama kumpa mtoto wao jina la ukoo. Wale wanaopinga mama kumpa mtoto jina la ukoo wa upande wa baba wanafanya unyanyasaji kwa kisingizio cha utamaduni, na hawaelewi hata kidogo maana ya moyo wa uhuru wa wanawake ni.

    Kiini cha moyo wa wanawake ni haki ya kuchagua njia za kuishi kwa uhuru, na kutokubali kunyimwa fursa mbalimbali kwa msingi wa jinsia. Na kutafuta haki yenye usawa ya wanawake pia hakulengi kuwachukia wanaume au ndoa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako