• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soko kubwa zaidi la biashara ya jumla ya mazao ya kilimo la Beijing lafungwa kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona(Sehemu ya kwanza)

    (GMT+08:00) 2020-06-18 16:35:28


    Habari kutoka Kituo cha kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya Corona cha Beijing zinasema, kuanzia tarehe 11 hadi 14 Juni, watu 51 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona, na wote ni watu wenye uhusiana na soko la Xinfadi ambalo ni soko kubwa zaidi la biashara ya jumla ya matunda, mboga na nyama mjini Beijing. Soko hili pia ni soko kubwa zaidi la mazao lenye thamani kubwa zaidi ya biashara barani Asia. Soko hilo sasa limefungwa.

    Soko la Xinfadi lililojengwa tarehe 16 Mei mwaka 1988, lina eneo la mita za mraba milioni 1.12, wasimamizi wa soko 1,500, na vibanda 2,000.

    Katika miaka 17 iliyopita, thamani ya biashara ya Xinfadi ilikuwa inaongoza nchini China kwa mauzo ya kilimo. Mwaka 2019, jumla ya thamani ya mauzo ilifikia yuan bilioni 131.9 (sawa na dola za kimarekani bilioni 18.62). Mbali na hayo, faharisi ya bei kwenye soko hilo pia imekuwa alama ya kuaminika kwa bei ya mazao ya kilimo nchini China.

    Daktari mwandamizi wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha China Bw. Wu Zunyou, amesema joto la chini na umati mkubwa wa watu ndani ya soko hilo vinalifanya soko hilo liwe na uwezekano wa kukumbwa na virusi vya Corona.

    Kwa upande mmoja, idadi kubwa ya bidhaa za nyama zinahitaji kuhifadhiwa katika mazingira yenye joto la chini, hali ambayo inaviwezesha virusi vya Corona kuishi kwa muda mrefu, na kuongeza fursa za maambukizi.

    Kwa upande mwingine, watu wengi wanaingia na kutoka kwenye soko hilo kila siku. Kutokana na hali hii, iwapo mtu mmoja mwenye virusi ambaye hajagunduliwa akiingia kwenye soko hilo anaweza kuwaambukiza wengine.

    Baada ya kufungwa kwa soko la Xinfadi, mji wa Beijing umepanga sehemu tano za muda za biashara ya mazao ya kilimo kushughulikia biashara ya mboga na matunda iliyokuwa inafanyika huko Xinfadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako