• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakazi milioni 2.3 wa Beijing wachukuliwa sampuli za vipimo vya virusi vya Corona

    (GMT+08:00) 2020-06-24 15:45:16


    Katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kazi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona uliofanyika tarehe 20 mjini Beijing, naibu mkuu wa kazi ya upimaji wa kikundi cha uongozi wa kazi ya kuzuia na kudhibiti maambukizi ya virusi hivyo Bw. Zhang Qiang, ameeleza kuwa tangu tarehe 13 Juni mlipuko wa virusi vya Corona ulipotokea kwenye Soko la Xinfadi, mji wa Beijing ulianza kukusanya sampuli ya wakazi. Hivi sasa madaktari 7,472 kutoka mashirika 59 ya ngazi ya pili na ya tatu ya matibabu, mashirika 28 ya upimaji wa upande wa tatu, na mashirika 20 ya udhibiti wa magonjwa wanashughulikia kazi ya kukusanya sampuli kwenye vituo 2,083 vya upimaji.

    Idadi ya watu wa kuchukuliwa sampuli za vipimo imeongezeka kutoka 8,000 hadi laki 5 kwa siku, uwezo wa upimaji umeongezeka kwa kiasi kikubwa. Hadi kufikia tarehe 20 Juni, watu milioni 2.3 walikuwa wamefanyiwa upimaji.

    Katika hatua hiyo, watu wanaoishi karibu na masoko yenye maambukizi ya virusi na mitaa iliyoko karibu na masoko hayo, pamoja na watu wanaoshughulikia migahawa, maduka makubwa, na masoko, usambazaji wa vifurushi walifanyiwa upimaji kwanza.

    Kwa mujibu wa maagizo ya mji wa Beijing, wakazi wa mitaa 40 ambayo imewekwa karantini hawaruhusiwi kutoka nje, na wakimaliza muda wa 14 wa karantini wanapaswa kufanyiwa upimaji tena, wale watakaothibitishwa kutokuwa na virusi wataweza kuondolewa kutoka kwenye karantini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako