• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Huduma ya "yaya ya mashamba" yapunguza wasiwasi ya wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini

    (GMT+08:00) 2020-07-13 10:03:15


    Bibi Li Suoju amepata njia mpya ya kilimo ya kutunza mashamba yake madogo ya ngano kwenye Kijiji cha Huishi ya wilaya ya Yicheng, mkoani Shanxi, bila ya kuathiri kazi yake katika mgahawa kwenye mji wa karibu.

    Kutokana na ustawi wa kazi za vibarua kupitia mtandao wa Internet, wakulima wa kizazi kipya ambao wanamiliki mashamba madogo wanaweza kutafuta njia nyingine za kulima shamba.

    Kulima shamba lenye Mu moja, sawa na moja juu ya 15 ya hektari moja ya ngano humletea Bibi Li yuan 400, (sawa na dola 56 za kimarekani), lakini humfanya awe na shughuli kwa karibu na nusu mwaka.

    Sasa kwa kutumia program ya simu ya mkononi, Bibi Li anaweza kumwajiri mtaalamu wa mashine ya shamba anayemsaidia kunyunyiza dawa za kemikali na kupanda mashamba yake kwa kulipa yuan 140, sawa na dola 20 za kimarekani. Kama watu wengine wengi ambao wana mashamba madogo wanataka kujihusisha katika maisha ya mijini, bila ya kuacha mashamba yao kijijini.

    Huduma kama hii ambayo inatajwa na wakulima kuwa ni "Yaya ya mashamba", inahusisha mchakato mzima wa usambazaji wa mbegu, kulima, kupanda, kupandishia, kuvuna hadi mauzo ya bidhaa.

    Jumla ya wakulima 13,000 kutoka vijiji 21 kwenye wilaya ya Yicheng, wanalima mashamba yenye eneo la Mu 80,000 kwa kutumia huduma hii, kiasi ambacho kinachukua asilimia 14 ya lile ya jumla ya ardhi wilayani humo.

    Wakati huo huo, ili kuhakikisha mapato ya wakulima, sera ya bima pia imeanzishwa, ambayo inahakikisha wakulima wapate faida ya yuan mia nne kila Mu, ili kuepukana na hasara kutokana na maafa ya kimaumbele na mavuno mabaya ya mazao. Kila mtu analipa yuan nane tu akaweza kupata malipo ya yuan 80, na pesa zinazobaki zinafadhiliwa na serikali.

    Mwaka huu, Yicheng itaendelea kuhusisha ardhi nyingi zaidi kwenye mfumo huo, ili kupunguza mizigo kwa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako