Hivi karibuni China imetangaza mpango wa kutoa mafunzo ya kiufundi kwa wafanyakazi za vibarua milioni 14 ndani ya miaka miwili, ili kukabiliana na ukosefu wa nafasi za ajira kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya ngvu kazi na utoaji wa huduma za kijamii, ndani ya mwaka mmoja ujao, watu zaidi ya milioni saba watapewa mafunzo hayo, nao ni pamoja na wafanyakazi za vibarua, wafanyakazi za vibarua ambao wamepunguzwa kazini, wahamiaji wapya kutoka vijijini, wafanyakazi za vibarua wanaorejea vijijini pamoja na wanavijiji maskini.
Maambukizi ya virusi vya Corona yameathiri vibaya wafanyakazi za vibarya milioni 290 nchini China, wengi wao wamekwamwa nyumbani kwao mwezi Januari. Wakati waliporejea mijini baada ya kuondolewa kwa karantini, ni vigumu kwao kupata ajira tena. Makadirio ya Gazeti la Economist yameonesha kuwa, idadi ya watu wasio na ajira nchini China ilifikia milioni 80 mwezi Machi, ambacho ni kilele cha kiwango hicho. Ripoti nyingine kutoka UBS imeonesha kuwa, idadi hiyo ilifikia milioni 70 had inane mwezi Machi na kupungua hadi kufikia milioni 33 hadi 40 mwezi Mei.
Mpango wa China wa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi za vibarua kutoka vijijini unalenga kuwasaidia watu hao wakati wanaporejea vijijini, ili kuwasaidia watafute ajira au kuanzisha biashara nyumbani kwao.
Kutokana na mpango huo, mafunzo hayo yatahusisha sekta za ujenzi, mashine, migahawa na usambazaji wa bidhaa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |