Hivi karibuni Bwana Xiao He amekuwa na masikitiko sana. Kwani ameanzisha uhusiano wa kimapenzi na mfanyakazi mwenzake, lakini baada ya uhusiano huo kugunduliwa na mkuu wake, alitakiwa kuondoka kutoka kampuni kutokana na kukiuka kanuni za ndani za kampuni.
Alitafuta ushauri wa kisheria, mwanasheria alimwambia kuwa, baadhi ya kampuni zina kanuni kuhusu "kutoruhusu wafanyakazi wenzi kuanzisha uhusiano wa kimapenzi au kufunga ndoa", la sivyo mmoja kati ya hao anapaswa kuondoka. Lakini mwanasheria amesema, kanuni kama hizo zikiwemo "kupiga marufuku wafanyakazi wenzi kufunga ndoa" au "mmoja kati ya wafanyakazi wenzi watakaofunga ndoa anapaswa kuondoka" hazina nguvu ya kisheria, kwani "uhuru wa ndoa" ni moja kati ya haki za kiraia zilizohusishwa kwenye katiba, ambayo haiwezi kuzuiliwa na kampuni yoyote. Pia ameongeza kuwa kanuni kama hizo si sababu ya kusimamisha makubaliano ya ajira. Ndiyo maana hata kama kanuni kama hizo zitapitishwa kwa utaratibu wa kidemokrasia au kutangazwa wazi hazifanyi kazi yoyote.
Hali kama hii vilevile imetokea katika nchi nyingine duniani. Hivi karibuni baadhi ya kampuni nchini Burundi zimepiga marufuku kuwaajiri jamaa za wafanyakazi. Na kampuni nyingine zimekataa kuwaajiri wafanyakazi wenzi waliofunga ndoa.
Wafanyakazi wa kampuni moja wanaotaka kufunga ndoa wanatakiwa kuhakikisha kuwa, mmoja kati yao anajiuzulu ndani ya miezi miwili ya ndoa yao. La sivyo mkataba wa mmoja wao utasimamishwa.
Wafanyakazi kadhaa walipohojiwa wamepinga hatua hiyo wakisema haihusishwi kwenye kanuni za ndani za kampuni, na pia imekiuka haki za binadamu, kwani kila mtu ana uhuru wa kuchagua mwenzi wake. Jambo linalosikitisha ni kuwa hatua hiyo ilitangazwa bila ya kujadiliana na Baraza la Kazi, ambalo hufanya kazi kama mpatanishi kati ya mwajiri na wafanyakazi kabla ya kuchukua uamuzi kama huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |