Baba mmoja mwenye umri wa miaka 26 wa mkoa wa Guangdong alimchukua binti yake aitwaye Dou Dou mwenye umri wa miaka minne na kusafiri hadi mjini Lhasa, mkoa unaojiendesha wa Tibet kwa baiskeli. Usafiri huu wenye umbali wa zaidi ya kilomita elfu nne ambao uliwachukua siku 71 uliwaachia kumbukumbu kubwa.
Baba huyo anaitwa Dou Haobei ana uzoefu wa kwenda mji wa Lhasa kwa baiskeli alioupata mwaka 2013. Kutokana na janga la virusi vya Corona, mwaka huu chekechea ya Doudou haikurejesha masomo. Ili kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Doudou, Dou Haobei aliweka mpango halisi kuhusu kumchukua na kusafiri naye hadi mji wa Lhasa kwa baiskeli.
Wakati wa usafiri huo, Dou Haobei alimchukua mtoto wake kutazama mashamba, vijijini, kutembelea maua na kando ya Ziwa Erhai, hata kupanda Mlima Dongda wenye urefu wa mita 5,130.
Bw. Dou amesema kusafiri huko ni zawadi kwa mtoto wake. Katika barua yake aliyoimwandikia mtoto wake alisema, anatumai mtoto wake afahamu somo muhimu la tabia la kushikilia kufanya jambo. Kuna umbali wa zaidi ya kilomita elfu nne kutoka mji wa Dongguan hadi mji wa Lhasa, na njiani kuna milima mikubwa kadhaa. Hata hivyo wameyashinda matatizo mbalimbali na kufanikiwa kufika eneo walilotaka kwenda. Hili ni somo muhimu katika maisha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |