• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kupiga marufuki matumizi ya mifuko ya plastiki isiyooza

    (GMT+08:00) 2020-08-17 17:15:04


    Idara tisa za serikali ya China, ikiwemo Kamati ya Mageuzi na Maendeleo, na Wizara ya Mazingira na Ikolojia, zimetoa taarifa ya pamoja kuhusu kusukuma mbele kazi ya kudhibiti na kushughulikia uchafuzi wa plastiki, na kuamua kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki isiyooza kwenye maduka na supamaketi katika miji yote ya China, kwenye shughuli mbalimbali za mikutano na maonesho na katika huduma ya kuagiza chakula mtandaoni kuanzia Januari mosi mwaka kesho.

    Hivi sasa mifuko ya plastiki imekuwa alama ya uchafuzi wa mazingira, hali inayoenda kinyume na madhumini ya mhandisi wa Sweden Bw. Sten Gustaf Thulin ambaye alivumbua mfuko wa plastiki mwaka 1959. Bw. Thulin alitarajia kuwa uvumbuzi wake utachukua nafasi ya mifuko ya karatasi ambayo inatumia raslimali nyingi za misitu, ili kuhifadhi mazingira ya asili ya Dunia. Anaona kuwa mifuko ya plastiki inapaswa kuwa na matumizi endelevu, na wala siyo kutupwa baada ya kutumiwa mara moja tu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako