• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijana afanya mazoezi ya "push-up" kando ya barabara ya mwendo kasi

    (GMT+08:00) 2020-08-11 16:08:02


    Katika majira ya joto, madereva wanaweza kusikia uchovu na usingizi baada ya kuendesha magari kwa muda mrefu, hali ambayo ni hatari sana kwa usalama wa barabarani.

    Alfajiri ya Juni 26, Polisi wa Usalama Barabarani mkoani Hubei walipofanya doria kwenye barabara ya mwendo kasi kati ya Shanghai na Chongqing, waligundua gari moja lenye usajili wa mkoa wa Zhejiang likiwa limeegeshwa kwenye Eneo la Maegesho ya Dharura (Emergency Parking Bay), huku kijana mmoja akifanya mazoezi ya Push-up kando ya gari hilo. Kijana huyo aliwaambia polisi alifanya hivyo ili kuondoa uchovu na usingizi baada ya kuendesha gari kwa muda mrefu wakati wa usiku.

    Polisi walimkumbusha kijana huyo kuwa Eneo la Maegesho ya Dharura kwenye barabara ya mwendo kasi ni kwa ajili ya hali ya dharura, na hatakiwi kuegesha gari lake kwenye eneo hilo bila kuwa na dharura yoyote. Pia walimwambia kuwa kufanya mazoezi kando ya barabara ya mwendo kasi ni kitendo cha hatari, na pia ni kinyume cha sheria. Hata hivyo, kwa kuzingatia kuwa kijana huyo alifanya hivyo kwa ajili ya kuhakikisha usalama wakati wa kuendesha gari, Polisi waliamua kutomwadhibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako