Kampuni moja ya China imemfukuza kazi mfanyakazi wake Bw. Yan kwa kutofanya kazi kwa saa nane kwa siku, na mfanyakazi huyo ameamua kuwasilisha mahakamani madai ya kurejeshewa mshahara wa ziada wenye thamani ya dola zaidi ya laki 7.1 za kimarekani tangu alipoanza kufanya kazi mwaka 2012 kwenye kampuni hiyo. Hata hivyo, madai yake yametupiliwa mbali na mahakama.
Bw. Yan alijiunga na kampuni ya Tencent mwezi Julai mwaka 2012, na kuwa mhandisi wa ngazi ya juu wa jukwaa la mchezo. Bw. Yan alisema makubaliano ya mwisho yaliyosainiwa kati ya pande hizo mbili ni kati ya tarehe 1 Oktoba mwaka 2015 na tarehe 30 Septemba mwaka 2021. Mwezi Machi mwaka 2019, kampuni hiyo ilisimamisha makubaliano na Bw. Yan kutokana na kukiuka nidhamu ya kazi.
Bw. Teng amesema tangu alipojiunga na kampuni hiyo, akiwa mfanyakazi wa IT ni jambo la kawaida kufanya kazi ya ziada baada ya saa kumi na mbili jioni, na hata hakupumzika wikiendi, lakini video ya kamera ya CCTV iliyowasilishwa na kampuni mahakamani haiwezi kuthibitisha muda wake wa kazi kwenye kampuni yake huanza saa nne mchana hadi saa kumi na mbili jioni. Kwa sasa, mfanyakazi huyu amewasilisha tena madai yake kwenye mahakama ya ngazi ya juu zaidi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |