Kama chakula ulichoagiza kimepotea utachukua hatua gani? Na ukiambiwa kuwa mtu aliyeiba chakula chako ni mwanafunzi wa chuo kikuu au mtu mwenye shahada ya kwanza, na wala siyo mwizi aliyefanya uhalifu mara kwa mara utakuwa na maoni gani?
Siku hizi, chakula cha kuagizwa kinapotea mara kwa mara kwenye eneo moja la makazi mjini Nanjing, na polisi wa huko walipokea ripoti ya kesi mpya na kufanya uchunguzi kwa makini.
Baada ya kuangalia kamera ya CCTV kwenye makazi hayo, polisi waligundua mwanaume mmoja alichukua chakula cha kuagizwa mara nyingi katika siku kadhaa zilizopita. Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa na polisi kutokana na kitendo chake cha wizi.
Habari za awali zinasema mwanaume huyo ni mwanafunzi wa chuo kikuu kinachojulikana, na sasa anajiandaa kushiriki kwenye mtihani wa wa shahada ya uzamili. Ana ndugu wanne katika familia yake, na kutokana na kuwa ana uhodari wa kusoma, ndugu zake wameacha masomo ili kuchuma pesa kwa ajili ya masomo yake.
Habari hiyo inafuatiliwa sana na watu. Baadhi ya watu wanaona mtu huyo alifanya hivyo kutokana na umaskini, na kwamba akiwa ni mtu mwenye shahada ya kwanza si nia yake kufanya kosa kama hilo.
Lakini kutokana na taarifa mpya zilizotolewa na polisi, mwanaume huyo si mwanafunzi wa chuo kikuu, bali alimaliza masomo chuoni miaka miwili iliyopita, na anakaa kwenye nyumba ya kupanga yenye mazingira mazuri, na kuwa na mapato ya kudumu. Alifanya hivyo kutokana na siku moja chakula alichoagiza kiliibwa na watu wengine, na anataka kulipiza kisasi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |