Kadiri kiwango cha mapato ya watu kinavyoinuka, ndivyo shughuli za usambazaji wa vifurushi zinavyopata maendeleo kwa kasi, na pia zimetoa nafasi nyingi za ajira. Takwimu zimeonesha kuwa, mwaka 2018 jukwaa la biashara ya kielektroniki la Meituan lilitatua suala la ajira kwa watu zaidi ya milioni 2.7 katika.
Hali inayofuatiliwa zaidi na watu ni kuwa, hapo awali watu walioshughulikia kazi ya usambazaji wa vifurushi walitoka vijijini, lakini kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni, kati ya watu milioni saba wanaoshughulikia kazi hiyo, zaidi ya asilimia 56 wana shahada ya elimu ya juu, na wale wenye shahada ya uzamili na ya juu zaidi wanazidi asilimia 1, na idadi hiyo imezidi elfu 70.
Takwimu hizo zinafuatiliwa sana na watu kwa sababu ni vigumu kwa watu kupata shahada ya juu, na wale wanaopata shahada ya juu wanatazamiwa kuwa nguvu muhimu ya kuchangia maendeleo ya kijamii, wala si kushughulikia kazi inayohitaji matumizi ya nguvu ya mwili, na kwa maoni ya watu wengi, hii ni hasara kwa watu kama hao na jamii.
Wengine wanaona hivi sasa idadi ya watu wenye shahada ya elimu ya juu inaongezeka, na ni vigumu kwao kupata ajira mwafaka, tena wanafunzi wenye shahada ya juu hawana mishahara mikubwa kuliko wale wenye shahada ya chini wakati walipohitimu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |